Friday, November 27, 2020

SH MIL 200 ZA YANGA ZAIVURUGA SIMBA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA MWANDISHI WETU


KAMA ulikuwa unajiuliza mara mbilimbili kwanini baadhi ya wachezaji muhimu wa Simba wamekuwa wakiweka ngumu kuongeza mikataba, sasa siri imefichuka kuwa ni ule mkwanja mrefu aliopewa Obrey Chirwa na Yanga.

Mashabiki wa Simba wamekuwa na wasiwasi mkubwa kutokana na baadhi ya wachezaji wao tegemeo kushindwa kuongeza mikataba yao kwa wakati, huku wakihusishwa kumendewa na Yanga na uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umegundua mengi.

Taarifa za ndani zinadai kuwa, baadhi ya nyota hao wa Simba wataka kuongezewa mishahara, kwani wanafanya kazi kubwa, lakini watu kama Chirwa wa Yanga ambao hawana lolote la ajabu wakilipwa fedha nyingi.

Chirwa alinunuliwa kwa Sh Mil 200 za Tanzania, huku taarifa zikidai kuwa kwa mwezi anapokea si chini ya Sh mil 7, kitu ambacho kinawafanya baadhi ya nyota wa Simba ambao wanaonekana kupambana sana msimu huu kuona hawatendewi haki.

Mpaka sasa wachezaji ambao wanatajwa kuwa wameweka ngumu kuongeza mikataba yao ni nahodha wa kikosi hicho Jonas Mkude, ambaye ni kati ya viungo bora kwa sasa hapa nchini pamoja na Ibrahim Ajib.

Mbali na wawili hao, mwingine ambaye inatajwa kuwa hajamalizana na klabu yake hiyo ni Said Ndemla, huku pia taarifa za uhakika kutoka kwa wekundu hao wa Msimbazi zikidai kuwa, walimwita Abdi Banda ili kumuongezea mkataba akagoma.

Taarifa hizo zinadai kuwa, Simba walimwita Banda wakazungumza naye kwa lengo la kumwongezea mkataba, lakini akawaambia kuwa mpaka akazungumze na meneja wake, ambapo taarifa zaidi zinadai kuwa huenda akakataa kabisa kusaini mkataba mpya.

Kuhusu Mkude, taarifa zinadai kuwa, anataka awekewe Sh milioni 80 mezani ili asaini mkataba mpya, huku Ajib naye akitaka zaidi ya hiyo, ambapo kwa upande wake Ndemla amewaambia wamuwekee mezani Sh milioni 60.

Taarifa zaidi zinadai kuwa, Mkude na Ajib wanawindwa sana na Yanga na kama Simba wakizembea tu kidogo inaweza ikala kwao, kwani wametengewa mzigo ambao wakiwekewa mezani hawawezi kuuachia.

Hata hivyo, kigogo mmoja wa Yanga ameliambia BINGWA kuwa kamwe hawawezi kumsajili Mkude, kwani msimu wa 2014 walimfuata wakiwa na kitita cha maana cha fedha akakataa, hivyo hawawezi kurudia matapishi.

“Msimu wa 2014 tulitembea na shilingi mil 80 mfukoni ili kumpa Mkude, lakini hakutusikiliza na badala yake akatudengulia, sasa kumsajili kipindi hiki ni sawa na kurudia matapishi, hatuwezi kufanya kazi hiyo,” alisema kigogo huyo wa Yanga

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -