Tuesday, November 24, 2020

SHEBBY LOVE: CHUKI CHANZO CHA MIKOSI BONGO FLEVA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA SHARIFA MMASI,

WAPENZI wa kazi za muziki wa Bongo Fleva nchini, wamezoea kumuita Shebby Love, lakini jina lake halisi ni Shaaban Seif, ambaye alianza kufahamika kwenye tasnia hiyo akiwa katika kundi la ‘Mkong’oto Juzz Band’, lililokuwa likiongozwa na mkali wa miondoko ya Hip Hop, Emmanuel Elibariki ‘Ney wa Mitego’.

Kupitia kundi hilo lililowahi kupata umaarufu miaka ya nyuma, lilifanikiwa kukuza jina la Shebby Love kwenye kiwanda cha Bongo Fleva hapa nchini, mara  baada ya Ney wa Mitego kumtoa Morogoro alikokuwa akiishi na familia yake.

Sababu kubwa ya Ney kumsafirisha msanii huyo kutoka mji kasoro baharina hadi jijini Dar es Salaam, ni kutokana na kiwango cha uimbaji alichokuwa nacho Shebby Love, kinachoendelea kuonekana hadi hivi sasa.

Ney wa Mitgo alizidi kumuamini Shebby Love mara baada ya umahiri wake aliouonyesha kwenye wimbo wa ‘Ukweli wa Moyo’ aliyoshirikishwa na Ney wa Mitego, ingawa ndoto yake kubwa kwenye sanaa ilianzia mbali kama anavyoelezea yeye mwenyewe.

“Wakati nipo shule  ya msingi Morogoro nilikuwa nikishiriki maigizo mbalimbali, nilipomaliza shule nilijikita kwenye biashara ndogo ndogo ambapo nilitumia fedha nilizokuwa nikizipata kwenda studio kurikodi nyimbo.

“Katika harakati za kutaka kutoka kimuziki nikiwa mkoani Morogoro, nakumbuka kuna siku nilikuwa nipo studio moja narikodi, mara akatokea Ney wa Mitego na kusikiliza baadhi ya ngoma zangu, na hapo ndipo ukawa mwanzo wa mimi na yeye kufahamiana.

“Namshukuru Mungu tulikubaliana mimi nayeye, ambapo alinichukuwa na kunileta jijini Dar es Salaam kuendeleza kipaji changu cha muziki, kinachoendelea kusumbua wakali wa Bongo Fleva hadi hivi sasa,” alisema Shebby Love.

Shebby Love anasema, kwa kipindi chote anachoendelea kutambulika na jamii kisanaa, amepata mafanikio mengi ikiwamo kuwa karibu na nyota wa kazi hizo akiwamo Ally Kiba, Diamond, Linah na wengineo.

Mbali na hilo, amesema amekuwa miongoni mwa wasanii wanaojizolea sifa nzuri kutokana na umahiri wa kazi zake na heshima nayoendelea kutoa kwa mashabiki wake bila kujali umri.

“Kupitia muziki ninaofanya ambao ndio kila kitu katika maisha yangu, nimefanikiwa mambo mengi sana ikiwamo kutambulika na wasanii wakubwa ndani na nje ya nchi, pia baadhi ya viongozi wa Serikali kwa hiki ninachoendelea kukifanya,” amesema.

Shebby  anasema popote kwenye riziki ni lazima kutakuwa na changamoto mbalimbali ambazo huwa zinatokea na kufanya maendeleo kuchelewa kufika kwa wahusika.

“Kwenye muziki hasa huu wa Bongo Fleva,  kuna chuki baina yetu sisi wasanii na hizo ndizo zinatuletea hata mikosi ya kushindwa kufanya kazi na wakali mbalimbali Kimataifa.

“Binafsi sifurahishwi na chuki hizo, kwa mwonekano  wa nje tasnia yetu inaonekana kuwa na sura nzuri lakini ndani imebeba majungu, fitina, chuki ambazo zinatufungia milango ya rizki bila sisi wenyewe kujua,” anasema Shebby.

Anasema chanzo cha chuki kwenye muziki huu wa Bongo Fleva, husababishwa na baadhi ya wasanii  wanaoleta makundi kwenye soko la muziki hali inayosababisha msukumo mkubwa kupungua kwa upendo baina ya mshabiki na wasanii na hata wenyewe kwa wenyewe.

“Sikubaliani kabisa na makundi yenye kuvunja amani ya muziki wetu, kwani ni sababu moja wapo itakayopoteza matumaini ya kimaendeleo kwenye soko la muziki hapa nchini,” anasema Barafu.

Shebby anaongezea kuwa kuwa ni lazima wasanii wavunje makundi yenye athari kwa maendeleo ya Bongo Fleva ili lengo la kuufikisha muziki wao Kimataifa litimie kwa asilimia kubwa.

Shebby anaendelea kufunguka kwa kuwataja wasanii mbalimbali anaowakubali hapa nchini, ambapo  moja kwa moja anamtaja mwanadada Linah huku akimsifia kuwa ni msanii mwenye kiwango cha Kimataifa.

“Kwa hapa nyumbani navutiwa na waigizaji wengi sana, lakini nachukuwa nafasi hii kumpa pongezsi na heshima kubwa mwanadada Linah kwa kazi nzuri anazozifanya,” amesema.

Anasema kwenye maisha yake ya sanaa, zipo kazi anazozifurahia na zingine anazikumbuka kutokana na mazingira ya ugumu wa kufanyia kazi aliyowahi kukumbana nayo.

“Mbali na kuendelea kufanya vema sokoni, ‘Utamu’ ni ngoma yangu mpya inayoendelea kutamba sokoni ambayo mimi mwenyewe naipa heshima kubwa sana kutokana na gharama nilizotumia kufanikisha kitu kizuri kama hicho.

“Nawashukuru sana mashabiki wangu kwa kuipokea kwa mikono miwili ngoma hiyo, kikubwa niwaombe wasichoke kuniunga mkono ninapotoa kazi nyingine ili nipate nguvu kubwa ya kuwapa kile wanachohitaji,” amesema.

Mkali huyu wa Bongo Fleva, ana mipango mingi kwenye tasnia hii, ikiwamo kufanya kazi zenye ubora ili aweze kuliteka soko la kimataifa.

“Muziki ndio ajira yangu, sina kazi nyingine zaidi ya uimbaji  ivyo ni lazima nihakikishe nafanya kazi zenye ubora wa hali ya juu ili niweze kulifikia soko la kimataifa ambalo wasanii wengi ndani na nje ya nchi, tunalitolea macho,” anasema Shebby Love.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -