NA KYALAA SEHEYE
MBUNIFU wa mavazi ya Kike Martin Kadinda, ameshinda na kutwaa tuzo ya kuwa mbunifu Bora wa Mwaka 2016, katika jukwaa la wabunifu la Swahili Fashion Week lililomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Tukio hilo lililojenga historia mpya ya Kadinda lilifanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam kwa siku tatu mfululizo, likiwa limeshirikisha wabunifu 25 kutoka nchi tano za Afrika.
Akizungumza na BINGWA, Kadinda alisema kuwa anamshukuru sana muandaaji wa jukwaa hilo Mustapha Hassanal kwani lengo lake ni kukuza vipaji wa ubunifu na wanamitindo.
“Nilianza kutambulika katika jukwaa hili miaka mitatu iliyopita na nimekomaa kupitia jukwaa hili hatimae nimekuwa mbunifu Bora, hii ni tuzo ya Afrika kwa kuwa jukwaa hili linashirikisha wabunifu kutoka Afrika,” alisema Kadinda.