Friday, December 4, 2020

Shida ya vijana wengi katika ndoa

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

Na Ramadhani Masenga

NDOA za vijana wengi wenye umri kati ya miaka 30 na kushuka chini nyingi zimevunjika na zile zilizo hai ziko katika hali mbaya sana.

Ni idadi ndogo sana ya ndoa nyingi za vijana wenye umri huo zina amani na furaha. Tatizo ni nini?

Tafiti mbali mbali zinaonesha kuwa hali hiyo inasababisha na mambo mbali mbali na machache kati ya hayo nitayajadili hapa leo.

1. Kutaka kuishi kama wako wenyewe

WENGI wanapoingia katika maisha ya ndoa akili na mitazamo yao hubaki kuwa ile ile kama vile bado wako wenyewe. Hali hii huchochea migogoro, visa na kusababisha ndoa nyingi kuyumba na hata kuvunjika.

Unaweza ukakuta mwanandoa iwe wa kike ama wa kiume anataka kuendelea na ratiba zake za kutoka usiku na marafiki kama ilivyokuwa zamani. Ama anataka kuamua mambo peke yake peke yake, wakati tayari katika maisha yake yuko na mtu mwingine.

Ni vema vijana wakajua. Baada ya kuamua kuingia katika maisha ya ndoa karibu kila kitu cha zamani kuhusu wao kinapaswa kubadilika. Hawapaswi kujiamua kama ilivyokuwa mwanzo na kila jambo lao la kimaisha pia linawahusu na wenza wao.

 2. Kutokuwa tayari kujifunza

HII iko zaidi kwa vijana wa umri wa miaka 18 mpaka 25. Vijana wengi kama ni mwanaume basi anajua majukumu yake pekee kwa mke wake ni kutafuta pesa ya kujikimu kimaisha na kujihusisha naye kimapenzi. Basi. 

Mambo mengine ya namna bora ya kuongea naye, kufanya mahusiano yake kuwa bora hajui na hajifunzi. Matokeo yake unaweza ukakuta anaendekeza zaidi marafiki zake ama mambo mengine na mwanamke wake akilalamika anamuita ana gubu kwa sababu anajiona anatimiza wajibu wake ipasavyo bila kujua  maisha ya ndoa yanahitaji zaidi ya kulala pamoja na kutafuta chakula cha familia.

Ama unaweza ukakuta binti kwa kuwa analala kitanda kimoja na mumewe, kwa kuwa anampikia chakula basi anajiona yeye ni mwanamke kamili bila kujua nafasi zake nyingine. 

Hajui kama mwanamke makini ni yule mwenye kufanya yote hayo aliyofanya kisha anakua na maarifa ya kumsaidia kumuweka sawa mumewe katika uelekeo wa maisha. Mwanamke makini ni yule mwenye kuwa tulizo halisi la mumewe dhidi ya mahangaiko ya Dunia.

Wanawake wanapaswa kujua kuwa mbali na kupika na kulala na waume zao ila wanaume wengi wanasumbuliwa na matatizo mengi ya kijamii ambapo wakirudi nyumbani wanataka faraja na kuona wakieleweka na wake zao. 

Sio mtu katoka kazini ila akirudi nyumbani anakutana na kero, maneno ya ovyo na karaha za kila namna.

Wanaume wako tayari kuvumilia mambo mengi ila si kuishi na mwanamke ambaye mdomo na kauli zake unakuwa kero na shida katika maisha yake.

3.  Washauri wabovu

NI sababu ambayo inapaswa kuangaliwa kwa umakini sana. Vijana wengi wa kike na wakiume wanaingia katika ndoa ila bado wahsuri wao wanabaki kuwa macheki bob na watu wasio ‘serious’ na maisha na wasio na maarifa ya kuosha kuhusiana na suala la mapenzi na ndoa kwa ujumla.

Ni vema  ikaeleweka, aina ya rafiki uliye naye anaweza akasababaisha maisha yako yakashika uelekeo wake. Hii inatokana na ukweli kwamba maisha yetu yanaathiriwa kwa karibu zaidi na watu tunaokuwa nao karibu kutokana tabia ya ubongo wa binadamu kubadilika kutokana na aina ya vitu ama watu tunaojihusisha nao muda mwingi.

Kijana akiingia katika ndoa anashauriwa kuepuka kutumia muda mwingi na vijana wasio na uelekeo wa kimaisha na zaidi wasiokuwa katika maisha ya ndoa. 

Hii inatokana na ukweli kwamba vijana wengi ambao hawako katika ndoa huchukulia mambo yao hasa ya kimahusiano katika namna nyepesi tofauti na watu walio katika ndoa. 

Kutokana na kuchukulia mambo ya kimahusiano kijuu juu kuna hatari sana hata na wao kumpa ushauri usiofaa ama akajikuta na yeye anaamua kama marafiki zake waamuavyo katika mambo yao.

4. Kujionesha nani zaidi

HILI ni kosa la msingi sana. Kijana wakiume akikosea anaona udhia kumuomba msamaha mwenzake kwa hofu ya kuonekana yuko rahisi (cheap). Halikadhalika msichana akimkosea mume wake anajishauri sana kumuomba radhi na kukiri kosa kwa kuona yeye ni bora zaidi kuliko mwenzake. Ujinga wa mtazamo huu umesababisha ndoa nyingi kufa.

Ndoa ni taasisi inayohitaji unyenyekevu, subra, kuombana msamaha na kusameheana. Haya yakikosekana kwa sababu wahusika wanajiona bora zaidi uhai wa ndoa husika unaweza kuwa mfupi zaidi kuliko maisha ya funza.

Instagram: g.masenga

Mwandishi wa makala haya ni mtaalamu mbobezi wa masuala ya ushauri wa uhusiano, maisha na utulivu wa hisia (Psychoanalyst)

“mailto:ramadhanimasenga@yahoo.com” ramadhanimasenga@yahoo.com

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -