Friday, October 30, 2020

Shilole alivyowazingua wanachuo Iringa na ‘say my name’

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA KYALAA SEHEYE

NOVEMBA 19 mwaka huu msanii wa muziki wa kizazi kipya, Zuwena Mohamed maarufu kwa majina lukuki, yakiwamo Shilole, Shishi Baby na Shishi Trump, amefanya makubwa katika Chuo Kikuu cha Tumaini, mkoani Iringa, kwenye shoo iliyopewa jina la ‘After Graduation Party’.

Kutokana na kutofahamu kuzungumza lugha ya Kiingereza fasaha, Shishi aliomba wanachuo hao kumfundisha pale alipotaka kuweka mbwembwe katika shoo hiyo ili kunogesha na kuleta ladha tofauti.

Katika shoo hiyo, Shishi aliwaonyesha kuwa tatizo si lugha ila yeye ni msanii wa muziki baada ya kufanikiwa kuwachezesha kisawasawa, akianza na ngoma yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la Nachuna Buzi aliyomshirikisha Man Fongo.

“Say my name Shishi women strong, au nakosea jamani, naomba kuelekezwa Kiingereza nimekuja kwa wasomi, nahitaji kufanya shoo kisomi zaidi ili tuweze kwenda sawa au nakosea?” Alisikika Shishi baada ya kupanda tu juu ya steji.

Baada ya kuanza na salamu hiyo, Shilole aliwachezesha mashabiki wake na kuanza na kibao cha Ukipata Buzi na Ulichune, kilichoshangiliwa vilivyo na wadada.

AANZA KUJIFUNZA KIINGEREZA

Baada ya kuimba nyimbo tatu mfululizo zilizonekana kuwapagawisha vilivyo wanachuo hao pamoja na shahada zao, alianza kutaka kufundishwa Kiingereza.

“Leo lazima niondoke humu nikiwa najua ‘kiinglish’ maana nimekuja kwa watu wenye ‘madegree’ na ‘maPhd’, sasa nina imani sitaondoka hivi hivi, naanza hapo ‘my name Shishi Trump’, niambieni basi nimalizie nini… ‘am music’ ndio ‘my work’… hapo vipi, naweza siwezi,” aliitikiwa kwa shangwe ‘unaweza na unajua sana’.

Dj wa klabu hiyo, Dj Edo, alichukua kipaza sauti na kumwambia Shishi: “Wewe unajua kabisa kuongea wengine wanaongeza ‘s’ mambo yanaisha, sasa wewe hapo unajua kujiita hadi jina lako, uko juu.”

Baada ya kuuliza maneno mawili matatu ya Kiingereza, Shishi alianza kwa kuwaambia, “nyie jifunzeni hiyo lugha yenu, mimi napanda ndege kwa kukata nyonga na kuwaburudisha, sasa ngoja niwaonyeshe kama Shishi wa kimataifa na Kiingereza changu kilipo.”

ANAANZA KUONYESHA KIINGEREZA CHAKE KILIPO

“Mimi sipandi ndege kwa kuongea, Kiingereza changu kipo na kinakubalika, nikianza kuimba na kucheza, basi hakuna atakayekataa kunichukua, subirini muone,” alisema na kuanza kufanya shoo ya hatari. Aliimba na kucheza nyimbo zake na baadhi za wasanii wenzake huku akishangiliwa na mashabiki kibao waliofurika ukumbini hapo, huku kuna wengine wakisema hawaamini kwani walikuwa wakimuona kwenye TV na mitandao ya kijamii.

Alifanya shoo na kuhakikisha watu wote wamepagawa na kila alipomaliza walimtaka arudi juu ya steji hadi ikabidi alazimishe kushuka.

Shoo hiyo ilisindikizwa na wasanii kibao chipukizi wa mkoa huo bila kumsahau mtangazaji na mchekeshaji maarufu wa Ebbony Fm ya Iringa King Mwalubadu ambaye alikuwapo katika usiku huo.

 WASANII CHIPUKIZI WAMZUNGUMZIA SHISHI

“Kwa kweli tumepata cha kujifunza muziki si lele mama na ustaa hautaki ubishoo,  Shilole leo ametufundisha namna ya kufanya kazi, wakati amependekezwa kuja katika onyesho hili kila mmoja aliguna na kudhani kuwa si mfanyaji kazi bali mpenda sifa ila amewadhihirishia anafanya kazi.

“Tumejifunza kitu kwa Shishi, ametupa ushirikiano mzuri na ametuonyesha namna ya kutawala jukwaaa kweli huyu hajaja kushangaa mjini, anafanya kazi,  maana amefanya kazi na imeonekana  tulikuwa hatuamini kama ni msanii, tulijua muuza sura ila leo kaukata mzizi wa fitina na Iringa nzima ameacha gumzo,” alisema Sadick Kiyeyeu ‘Dick yeye’.

Katika hilo, Shishi aliliambia BINGWA kuwa kila anapokwenda kufanya shoo huwa haibii mtu, anafanya kazi kwa kuwa lengo la maisha yake ni kufanya kazi hivyo hataki kupoteza fursa hizo.

“Natafuta pesa (fedha) na si kitu kingine, hivyo nikipata fursa, sina budi kufanya kazi ili kujijengea heshima siku nyingine uitwe na si kuzunguka zunguka na kujiharibia jina… unadhani mashabiki wakikuponda utapata wapi tena fursa ya kufanya kazi? Mimi najitangaza kwa kazi na nina uhakika nitafika ninapopataka kwa kuwa natumia sauti na mwili wangu kuwapagawisha mashabiki,” alisema Shilole.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -