Thursday, October 22, 2020

Shime, Matola watajwa kumrithi Julio

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA WINFRIDA MTOI

KLABU ya Mwadui imeanza kuwawania makocha watatu,  Seleman Matola, Bakar Shime na Salum Mayanga, kwa ajili ya kuifundisha timu yao inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, baada ya Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ kuachia ngazi.

Julio alifanikiwa kuipandisha timu hiyo daraja msimu uliopita na hivi karibuni alitangaza kuachia ngazi kwa madai ya kuchoshwa na uamuzi mbovu wa waamuzi.

Akizungumza na BINGWA jana mmoja wa viongozi wa kamati ya klabu hiyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alisema makocha wengi  wametuma maombi kutaka kuinoa timu yao.

Kiongozi huyo alisema pamoja na  kujitokeza makocha wengi, lakini wanaopewa nafasi kubwa ni watatu ambao ni Matola, Shime  na Salum Mayanga wa Mtibwa Sugar.

Wengine wanaotajwa kumrithi Julio ni Mrage Kabange aliyekuwa kocha msaidizi wa JKT Ruvu, Yusuf Chipo raia wa Kenya na aliyewahi kuinoa Coastal Union, Oscar Mirambo na Denis Kadito.

Katibu Mkuu wa Mwadui, Ramadhani  Kilao, alisema bado wanaendelea kupitia maombi yanayotumwa na makocha hao hadi mwishoni mwa wiki hii.

“Najua kipindi hiki kila mtu ataongea lake, maombi tuliyonayo ni mengi na bado tunapitia CV zao tukimaliza kama wapo wakipendekezwa tutamwita mmoja mmoja kuzungumza naye,” alisema Kilao.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -