Sunday, November 29, 2020

SHIME: TUMEJIPANGA KUIBEBA TANZANIA AFCON

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAINAB IDDY

TIMU ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys, imeweka kambi katika hosteli za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ikiwa na wachezaji 30.

BINGWA lilimtafuta kocha wa timu hiyo, Bakari Shime, kuzungumzia maandalizi ya kiufundi ya timu hiyo kuelekea mashindano hayo.

Shime ameonyesha pia furaha zake kwa timu hiyo kufanikiwa kutinga kwenye mashindano hayo pamoja na mikakati yao kuifikisha mbali na kuipeperusha vema bendera ya Tanzania kimataifa.

Alivyoipokea taarifa ya kufuzu

Kocha huyo anasema alifurahi kuona timu yake imefuzu kushiriki mashindano hayo makubwa Afrika, kwani kwa miaka mingi Tanzania imekosa nafasi hiyo.

Anasema kufuzu kwa Serengeti Boys ni ishara tosha kuwa Mungu amesikia kilio chao na kuyaona machozi yao yaliyomwagika katika vipindi viwili tofauti, mara baada ya kutolewa baada ya kufungwa na Congo.

“Roho iliniuma nilipoona vijana wadogo wenye nia ya kuipa mafanikio Tanzania wakitokwa machonzi nchini Congo baada ya kutolewa, lakini pia hali hiyo ilijirudia tena siku ya kupongezwa hapa nyumbani, binafsi nilitokwa na machozi kwani dhahiri ilimuumiza kila mmoja wetu.

“Nashukuru Mungu ameweza kuona machozi ya vijana hawa wadogo na kwa kuwa anatenda haki aliweza kuwapa haki ya kushiriki mashindano hayo, sina shaka na watoto wetu na nina hakika watafanya vizuri, kwani kwa muda mrefu tumekuwa tukihangaika kucheza fainali hizi kwa ngazi ya vijana.”

Mabadiliko ya kikosi

Anasema mashindano yanahitaji wachezaji 21 na katika kikosi chao kilichoiwezesha Serengeti kufuzu wamebaki 18 kutokana na watatu kuvuka umri unaohitajika kwenye mashindano hayo na hivyo kuonekana wazi tayari kuna upungufu.

Kutokana na hali hiyo, Shime amesema kwa sasa anamalizia mechi mbili au tatu katika kikosi cha JKT Ruvu, kabla ya kuungana timu hiyo ili kuangalia wachezaji waliongezwa kutoka kwenye mashindano ya Artel Rising Stars na Klinik iliyoendeshwa na TFF.

“Kwa taarifa nilizonazo, kuna wachezaji 12 wapya ambao nitakapojiunga na timu nitaanza nao ili kuona akina nani wanaweza kupata nafasi ya kujiunga na Serengeti ili kufidia wale waliopungua.

“Taratibu za CAF zinasema orodha ya kwanza wanatakiwa wachezaji 23 na ya mwisho 21, kwa sasa wapo 18 na wale tuliowaongeza 12  kama wataridhisha tutawajumuisha na kuwa kikosi kimoja lengo ni kupata timu yenye ushindani na itakayoweza kuleta furaha kwa Watanzania,” anasema.

Upimwaji wa afya

Kuhusu kupimwa afya kwa wachezaji Shime anasema: “CAF itawapima wachezaji wao kipimo cha MRI kabla ya kuanza fainali, lakini kwa wale 18 wa zamani hawana tatizo kwani walikuwapo katika kampeni ya kufuzu umri wao haujazidi miaka 17.”

Jumamosi wachezaji wapya wote walikwenda Hospitali ya Muhimbili kwa ajili ya vipimo vya afya na umri na majibu yatatoka wiki ijayo.

Kundi la Serengeti Boys

Katika fainali hizo, Serengeti imepangwa katika kundi B na timu za Angola, Niger na mabingwa watetezi Mali  na katika hilo Shime anasema: “Mpira ni jinsi unavyojiandaa kimwili na kiakili, kama hatua ya kufuzu tumeweza  kuvuka sina shaka kwa maandalizi tunayofanya tutaweza kufika katika mafanikio ya kuweza kushiriki fainali.

“Kwa sasa timu iko kambini na programu zote zinaendelea,  ninapata taarifa ya kipi kinaendelea kutoka kwa mshauri wa ufundi, Kim Poulsen na nina uhakika hakuna kitakachoharibika kwani baada ya muda mfupi kutoka sasa nitaenda kuungana nao ili kuongeza nguvu,” anasema Shime maarufu kama Mchawi Mweusi.

Wakati huo huo, kocha msaidizi wa timu hiyo, Oscar Milambo, anasema Serengeti kwa sasa inafanya mazoezi asubuhi na jioni kwenye Uwanja wa Karume ambako timu hiyo imeweka kambi lakini inatarajia kupumzika kwa wiki mbili kabla ya kwenda kujichimbia nje ya nchi ambako Serikali itapendekeza waende.

“Mara baada ya kurejea kutoka kwenye mapumziko ya wiki mbili, tutaweka kambi nje ya nchi pamoja na kucheza mechi za kirafiki kulingana na mapendekezo ya kocha mkuu na mshauri wake,” anasema.

Milabo anasema kikubwa wanahitaji sapoti kutoka kwa wadau kwani timu hiyo imekuwa ikitegemea kila kitu kutoka katika shirikisho.

“Ni wakati wa kila Mtanzania kutuunga mkono katika kuhakikisha Serengeti inakuwa na maandalizi mazuri kutokana na ugumu wa timu tunazokwenda kukutana nazo,” anasema.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Vijana ya TFF, Ayoub Nyenzi, anasema kuwa kwa mara ya kwanza Tanzania imeanza kujenga bomba la mtiririko sahihi wa maendeleo ya vijana.

“Kwa miaka mingi Tanzania imekuwa ikisaka mafanikio ya soka kwa kuanzia juu kwenda chini na mara zote imefeli, kuna utofauti sasa na hii ndio njia sahihi, kuwekeza kwa kuanzia chini kupata bomba la mtiririko wa maendeleo ya soka nchini,”anasema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -