Friday, October 23, 2020

Shiza Kichuya ‘From zero to hero’

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA HUSSEIN OMAR

‘KUPANGA ni kuchagua’, kauli rahisi unayoweza kuitumia kama msemo katika mazingira ya kawaida yanayozunguka maisha ya kila siku yaliyoambatana na changamoto nyingi kwenye utafutaji riziki wa mwanadamu.

Agosti 20 mwaka huu pazia la Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara (VPL) lilifunguliwa kwa klabu 16 kushuka kuanza kuchuana kuwania ufalme wa soka nchini kwa msimu wa 2016-17.

Tangu kuanza kwa msimu huu kumekuwa na matukio mbalimbali ya kufurahisha na kustaajabisha miongoni mwa wachezaji wanaoshiriki kwenye ligi hiyo wakiwa na timu zao.

Moja kati ya matukio ya kuvutia yaliyotokea kwenye VPL msimu huu na yatakayobaki kwenye vichwa vya watu kwa muda mrefu, ni bao la winga wa Simba, Shiza Kichuya alilofunga dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga, Oktoba mosi mwaka huu.

Kichuya ambaye alikuwa shujaa kwenye pambano hilo, usajili wake Simba haukuwa wa mbwembwe kulinganisha na wenzake kama akina Laudit Mavugo, Fredirick Blagnon na wengine, lakini siku zinavyozidi kwenda anazidi kuwa kipenzi cha mashabiki wa timu hiyo ya Msimbazi.

Kwenye makala haya BINGWA linatazama safari ya Kichuya kutoka kuwa mchezaji wa kawaida hadi shujaa (from zero to hero), huku jina lake likiwafunika hata mastaa wa VPL kama akina Donald Ngoma, Amis Tambwe, Ibrahimu Ajib, Mavugo na wengineo.

Huyu ndiye Kichuya

Kichuya ni mmoja kati ya mawinga wachache mafundi wa kutumia mguu wa kushoto ambaye anatikisa soka la Tanzania kwa sasa kutokana na kipaji chake cha hali ya juu cha upigaji krosi, chenga za maudhi na mtaalamu wa kupiga pasi za mwisho.

Jina la Kichuya halikuwa maarufu kabla ya michuano ya Kombe la Mapinduzi Januari mwaka huu, lakini kiwango chake katika michuano hiyo akiwa na kikosi cha Mtibwa ndicho kilichompandisha na kumfanya kuwa gumzo nchini.

Katika michuano hiyo ya Mapinduzi, Kichuya alifanya mambo makubwa kutokana na uwezo wake uwanjani kiasi cha kuzivutia klabu za Simba, Yanga na Azam ambazo zilianza kupigana vikumbo kusaka saini yake.

Simba yamsajili, yampa jezi ya Okwi

Vita ya kusaka saini yake ilimalizwa kwa Simba kuibuka washindi baada ya kumsajili na kumfunga na mkataba wa miaka miwili, huku ikidaiwa kuwa alilamba dau la shilingi milioni 20 kwa fedha za usajili.

Siku chache baada ya kusajili Simba, Kichuya alipewa jezi namba 25 ambayo inaheshimika sana Msimbazi kutokana na kuwahi kuvaliwa na nguli wa zamani wa timu hiyo, Mganda Emmanuel Okwi.

Baada ya kukabidhiwa jezi hiyo baadhi ya mashabiki wa Simba walianza kuhoji iwapo ataweza kuitendea haki, lakini baada ya mechi saba tu za msimu huu kila mtu sasa anakubali kuwa staa huyo anastahili kuvaa jezi hiyo.

Kuhusiana na jezi hiyo, Kichuya mwenyewe anasema: “Jezi hii ni kubwa sana kwangu, lakini naamini kwa uwezo niliopewa na Mwenyezi Mungu ni wakati wangu mwafaka kuivaa na nina imani kwa uwezo wake nitaitendea haki.”

Amjibu Kaburu kwa vitendo

Kabla ya Kichuya kukabidhiwa jezi namba 25, Makamu wa Rais wa Simba, Godfrey Nyange ‘Kaburu’, alimchana ukweli juu ya heshima ya jezi hiyo.

“Hii jezi ina heshima kubwa sana Simba tunakupa wewe Bwana mdogo, nenda kaitendee haki, aliyekuwa akiitumia jezi hii alikuwa ni mtu hatari ambaye hadi sasa hakuna mfano wake na kama hutaitendea haki tutakubadilishia,” alisema Kaburu siku akimkabidhi Kichuya jezi hiyo.

Lakini hadi sasa inaonekana kama Kichuya ameamua kujibu maneno ya Kaburu kwa vitendo kutokana na kuonyesha kiwango cha juu sana akiwa na jezi hiyo, kitu kinachothibitisha kuwa anastahili kuvaa jezi hiyo.

Maisha yake yamebadilika

Mechi saba alizoichezea Simba na kuifungia timu hiyo mabao matano zimetosha kubadilisha mfumo wa maisha ya Kichuya, kutokana na kuishi kifalme katika timu hiyo yenye maskani yake Mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam.

Hakuna ubishi kuwa Kichuya hivi sasa ndiye staa wa Simba, hii inatokana na juhudi zake binafsi uwanjani huku akiwa na chachu kubwa ya kufika mbali kutokana na kipaji alichonacho.

“Bado nina safari ndefu, najua nini nafanya, nimekuja mjini kutafuta, nitapigana kufa au kupona kuhakikisha nalinda kipaji changu na kuisaidia timu yangu kufika mbali,” anasema Kichuya.

Haogopi changamoto

Kichuya anasema pamoja na mafanikio machache aliyonayo anajiona kama ni mtu mwenye bahati kutokana na nyota yake kung’ara katika kipindi kifupi akiwa na Simba.

Kutokana na hali hiyo anasema pia yupo tayari kukabiliana na changamoto mbalimbali atakazokutana nazo ikiwemo ile ya kuzomewa na mashabiki uwanjani pindi inapotokea anacheza vibaya.

“Nipo tayari kukabiliana na changamoto zote, kuzomewa, kushangiliwa ni sehemu ya maisha yetu sisi wachezaji, nimejipanga kisaikolojia na hali hiyo pia nipo tayari kukabiliana nayo wakati wowote itakaponitokea,” anasema Kichuya.

Siri ya mafanikio

Kichuya anasema mafanikio yake yanatokana na nidhamu ndani na nje ya uwanja ikiwa ni pamoja na kujituma muda wote akiwa mazoezini ndio maana haikuwa ajabu kwa benchi la ufundi la Simba linaloongozwa na Joseph Omog kumpa nafasi katika kikosi cha kwanza.

“Siri ya mafanikio ni kujituma, kujiheshimu na nidhamu kwa makocha ambao siku zote wanapenda wachezaji wenye tabia hizi hivyo akili kichwani mwako,” anasema.

Kichuya anasema siku zote anahitaji marafiki wanaompa ushauri mzuri aweze kutimiza malengo yake ikiwemo kuachana na mambo ya kidunia na kujikita zaidi kudumisha kiwango chake.

Awapoteza Cheka, Afande Sele

Kichuya ndio habari ya mjini kwa sasa katika vitongoji mbalimbali vya mji kasoro bahari, Morogoro, kutokana na bao lake maridadi alilolifunga akiisawazishia timu yake ya Simba dhidi ya Yanga, Oktoba mosi, Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Enzi za ufalme wa bondia Francis Cheka na mwanamuziki Afande Sele, ni kama zimekwisha katika vitongoji vya Mafiga,Tanesco, Kihonda, Mji Mpya, Msamvu, Boma Road, Forest, Mzumbe na Sua kutokana na umaarufu wa Kichuya alioupata hivi karibuni.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -