Tuesday, November 24, 2020

SHUKRANI MKWASSA, BAKI NA UKWELI WAKO MOYONI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA AYOUB HINJO

SIKU zote ukisema ukweli unamfanya mtu kulia ni vizuri kuliko kusema uongo na kumfanya mtu atabasamu. Ukweli na uongo ndio maisha yetu ya kila siku katika uso wa dunia hii.

Hakuna kitu kizuri kwenye maisha kama kuusikiliza uongo lakini ndani yake ukweli wote unaujua. Kwa heri Mkwassa. Sisi Watanzania wenzako tuko pamoja nawe.

Mkwassa hakufikia mwisho wa uwezo wake wa kuifundisha timu ya Taifa ya Tanzania, hakuna asiyefahamu hilo. Kadiri muda ulivyokuwa unasonga Mkwassa alionekana kuchoka.

Si kuchoka kiuwezo wala kiakili, moyo wa Mkwassa ulikuwa na mengi yanayoumiza kuliko kufurahisha, alibaki akilia yeye na moyo wake.

Timu yetu ya taifa ina matatizo mengi kuliko inavyoonekana lakini Mkwassa aliyabeba na kuyahifadhi moyoni mwake.

Siku zote chuki humchoma anayeihifadhi. Mambo mengi sana ya Mkwassa yalionekana kukwama lakini kukaa kwake kimya kumesababisha matatizo mengi kutokea.

Rekodi yake si yakufurahisha akiwa na Stars. Michezo 13 aliyoiongoza timu ya taifa ameshinda mara mbili pekee, kufungwa sita na kutoa sare tano.

Wamepita makocha wengi kwenye timu ya Stars lakini mafanikio hayaonekani. Unadhani mafanikio waliyonayo Misri, Nigeria, Ghana na wengine yalitokea kwa bahati? Tatizo lipo lakini tumelificha na matokeo yake limekuwa kubwa lisiloweza kutatulika kirahisi.

Hivi sasa tunaitazamaje timu ya Cape Verde? Timu ambayo ilikuwa kama chakula kwa Stars lakini kwa sasa si daraja letu tena. Kufanya kwao vizuri ni kutokana na kuambiana ukweli.

Wakati mwingine kuuficha ukweli kunasababisha mambo mengi yenye matatizo kutokea. Kukaa kimya kwa Mkwassa kumeleta athari kwa timu yetu kushindwa kuendelea na kujikuta tukishuka kila siku. Lakini pia kumefanya kuharibu wasifu wake kwa kiasi kikubwa. Kocha gani anashinda mechi mbili kati ya 13? Kwa watu wasioangalia ubora na wanaoangalia matokeo Mkwassa amechafua wasifu wake vibaya mno.

Ukimya wa Mkwassa umetufikisha hapa ambapo Stars inaonekana ipo juu ya timu 6 kutokea mwishoni kwenye viwango vya timu za taifa kwa mujibu wa CAF.

Ukweli ilitakiwa usemwe mapema. Miezi kadhaa nyuma Mkwassa aliwahi kulalamika ratiba zake na programu zake zinashindwa kwenda sawa sababu hakuna anayejali.

Kuondoka kwake kutaturudisha nyuma zaidi sababu itatulazimu kuanza upya wakati mwaka 2019 ulitakiwa kuwa mwaka wa Stars kufuzu kucheza mataifa ya Afrika (AFCON).

Programu mpya zitakazoletwa na kocha mwingine siamini kama zitatufikisha popote ikiwa hawa waliopita kila mmoja analalamikia uongozi.

Hivi tunawaangaliaje Uganda kwa hatua waliyofikia? Zuri linaigwa lakini kwetu ni tofauti hadi kufikia hatua ya mashabiki kuisusa timu yao.

Mkwassa ni kocha mzawa ambaye alikuwa na malengo ya kufunika rekodi za makocha wa kigeni. Kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2018, michuano ya Chan na AFCON vyote vilikuwa kwenye mipango yake.

Si rahisi kwa wengi kumkumbatia Mkwassa wakimuona mtaani kinyume chake atatukanwa kwa kuifanya Stars kuendelea kuwa timu kibonde zaidi.

Mkwassa kapitia mengi ya kuumiza kuliko kufurahisha kwenye kazi yake na Stars. Tumwache aondoke zake sababu alishaumia vya kutoka na anaondoka na majeraha ya moyo na majeraha ya CV yake kuhabarika.

Hivi ni nani anayeweza kufanya kazi bila malipo? Kinachomuumiza zaidi Mkwassa ni kuona suti kali za viongozi wa TFF zikivutia machoni mwa watu huku fedha nyingi na nyingine zikielekezwa kwenye harakati za uchaguzi wa TFF unaoendelea.

Masahibu aliyopitia Mkwassa yawe mwisho. Siasa za soka ndani ya TFF ziwe mwisho. Tatizo tumezoea kuishi kwa mazoea na kujuana.

Mzigo alioubeba Mkwassa ulikuwa mzito, ulikuwa umeshamzidi uzito angelazimisha kuubeba angeanguka nao hata nafasi ya kunyanyuka tena asingeipata.

Hata Roma haikujengwa kwa siku moja. Kila mtu anamnyooshea kidole Mkwassa, tunamwonea katika hili. Wapo walioshika mpini huku yeye akishika makali sasa wamemuumiza kwa kulazimisha kuvuta.

Muda huu ni wa kujitathimini wapi tunakoenda. Lazima tukubali kuanza upya kwa kujenga misingi imara kwa wachezaji wetu kuanzia ngazi za watoto ili kuijenga timu bora na imara ya taifa.

Serengeti Boys hao wapo kwenye barabara nzuri, wanachohitaji ni kusimamiwa vizuri. Tuanze nao kuisuka Tanzania mpya.

Mkwassa asante kwa yote. Lakini wakati mwingine kukaa kimya kunaharibu mambo mengine.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -