Saturday, November 28, 2020

SI KAZI ZA NJE, BONGO MOVIES MJIPANGE

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAITUNI KIBWANA,

WIKI hii, Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam, alitoa siku 10 kwa wote wanaojihusisha na  biashara isiyo halali ya ‘kudownload’ filamu na kazi za wasanii jijini waache mara moja, kwani baada ya siku hizo wataendesha msako wa kuwakamata wote watakaokuwa bado wanajihusisha na biashara hiyo.

Lakini pia wale wauzaji wa filamu za nje wametakiwa kuachana na biashara hiyo mara moja kabla ya siku hizo kukamilika, huku zile filamu za utupu zikipigwa marufuku na hatua zitachukuliwa kwa wale wote wanaosambaza kwenye vibanda visivyo rasmi.

Agizo hilo liliungwa mkono na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, ambaye ametilia mkazo sakata hilo kwa kusema kuwa hatua hizo ni utekelezaji wa sheria mbalimbali za nchi  yenye kusimamia filamu na ile ya hakimiliki na hakishiriki.

Maagizo hayo yanakuja baada ya wasanii kuilalamikia Serikali kwa kushindwa kuwalinda wao na kazi zao kwa kuruhusu filamu na tamthiliya za nje kuingia kwa wingi nchini na hivyo kuzidi kuwadidimiza.

Moja ya sababu ambazo zimekuwa zikitajwa na wasanii wa Bongo Movies kama chanzo cha kuzorota kwa soko la kazi zao, ni  kitendo cha kazi za nje kuingizwa kiholela nchini, huku zikiuzwa kwa bei chee hivyo kuzigharimu zao.

Lakini wakati wasanii hao wakilalamikia kazi za nje, wapo wadau wa filamu wanaoliangalia hilo kwa jicho la pili kwamba kuzorota kwa kazi za wasanii wa hapa nchini kumetokana na kubweteka kwao.

Wadau hao wamekuwa wakidai kuwa wasanii wetu wamekuwa wakitoa kazi zisizo na ubora, kuanzia katika utunzi, uigizaji na zaidi, ikiwa ni wasanii kushindwa kuuvaa uhusika ipasavyo.

Ni kutokana na kasoro hizo, imeelezwa wapenzi wa filamu nchini wamejikuta wakitekwa kirahisi na filamu na tamthiliya za nje ambazo zimekuwa katika ubora wa hali ya juu.

Miongoni mwa kazi za nje ambazo zimetokea kuwabamba vilivyo wapenzi wa sanaa wa Bongo ni tamthiliya ya Udaan Sapnon Ki iliyochezwa na wasanii wa India, akiwamo binti mdogo aliyeonyesha ubora wa hali ya juu, Spandan Chaturvedi ‘Chakor’.

Kwa sasa tamthiliya hiyo imeonekana kuwabamba vilivyo Watanzania kutokana na ubora wake kiasi kwamba katika vibanda au maduka yanayouza kazi za filamu, imekuwa ikinunuliwa kwa wingi mno.

Ni kutokana na kufahamu hilo, wasanii wa hapa nchini wamekuwa wakipiga kelele kuitaka Serikali kupiga marufuku uingizaji wa kazi za nje ili kulinda soko lao, ila ukweli ni kwamba hakuna asiyejua kwa sasa soko la filamu limeshuka na tunazidiwa kwa kiasi kikubwa na wasanii wachanga wanaozaliwa huko Nigeria kwa sababu tu, wenzetu wamejenga misingi imara ambayo iliundwa na wasanii wakongwe.

Ifahamike kuwa iwapo wasanii wa Bongo Movies wataandaa kazi nzuri ambazo zitakuwa na ujumbe mwanana kwa jamii, wahusika kuvaa uhusika wao kama ilivyotakiwa, huku kazi zao zikiwa na mwanzo na mwisho unaoeleweka, hakuna atakayeziacha na kukimbilia zile za kigeni zilizochezwa kwa lugha za kigeni huku baadhi ya wale wanaozitafsiri ‘wakichapia’.

Bongo Movies wanapaswa kujiuliza kwanini awali soko la filamu lilishika kasi na leo hii linaburuza mikia, watu wamechoka kununua kazi ambazo hazina mvuto, hadithi zile zile hata sauti ni unga unga mwana.

Kama mnahitaji kuuza kazi zenu mnapaswa mbadilike, mjitathmini na muwe wabunifu mnaweza kufanikiwa, lakini hili la kuzuia tu alafu ladha ni zilezile kwa kweli mtaendelea kusugua benchi tu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -