Thursday, November 26, 2020

SI RONALDO WALA MARCELO, CASEMIRO ANATOSHA…

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

MADRID, Hispania

BAADA ya kupona majeraha yake kiungo mkabaji wa Real Madrid, Casemiro, amecheza kila dakika ya mchezo wa timu yake hiyo na mara zote hizo hajamwangusha kocha wake Zinedine Zidane, ambaye amepumzisha wachezaji wengine wote kikosini mwake tangu Mbrazil huyo alivyorudi.

Madrid inakabaliwa na mechi muhimu za La Liga na Copa Del Rey na Zidane ameweka wazi dhamira yake ya kusimamia sera yake ya kuwapumzisha wachezaji wake kwa muda stahiki, lakini sera hiyo imegonga mwamba kwa Casemiro.

Mbrazil huyo hakuonekana dimbani katika michezo 13 kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya mfupa wa mguu uliovunjika na aliporudi alianzia benchi dhidi ya Sporting, akacheza dakika 90 dhidi ya Cultural kwenye Copa del Rey kabla ya kumalizia dakika 25 dhidi ya Barcelona pale Camp Nou.

Alipata nafasi ya kucheza kwa dakika 90 dhidi ya Deportivo, Granada na Sevilla katika mechi za La Liga. Akacheza dhidi ya America na Kashima Antlers kwenye michuano ya kuwania Kombe la Klabu Bingwa ya Dunia na akacheza tena dhidi ya Sevilla kwenye Kombe la Copa del Rey.

Kwenye mtiririko huo wote wa mwezi na nusu uliopita, Zidane amewapumzisha wachezaji wake wengine kama Keylor Navas, Cristiano Ronaldo na Luka Modric, ambao hapo kabla walionekana kama si wachezaji wa kupumzishwa.

Dani Carvajal, Karim Benzema na Marcelo pia wamepigwa benchi kwa nyakati tofauti.

Sergio Ramos na Lucas Vazquez pia walikaa benchi kutokana na majeraha yaliyowakumba miezi michache iliyopita.

Madrid walitarajiwa kukipiga jana na Celta Vigo kwenye mchezo wa Copa del Rey, ushindi kwenye mchezo huo utakifanya kikosi cha Zidane kuwa na ratiba ngumu baadaye itakayokuwa na mechi mbili kila wiki hadi Machi mwaka huu, hali itakayomlazimu Zidane kufikiri sana namna ya kuwapa wachezaji wake muda wa kutosha wa kupumzika.

Na kwa kiasi fulani Casemiro naye atapata nafasi ya kupumua.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -