Thursday, October 22, 2020

Sia Pius; Miss Sinza 2016 aliyepania kubeba taji la Miss Tanzania

Must Read

Wanaompenda Carlinhos wapewa dili

NA ASHA KIGUNDULA      MASHABIKI na wanachama wa Yanga, wakiwamo wale wanaovutiwa mno na uchezaji...

UKITELEZA KWISHNEI

NA ASHA KIGUNDULAMIAMBA ya soka nchini, Simba na Yanga, leo wana vibarua vigumu vya kusaka pointi zote...

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

NA BEATRICE KAIZA

KUELEKEA shindano la Miss Tanzania 2016 ambalo washiriki wake wanatarajiwa kuingia kambini Ijumaa hii, Miss Sinza 2016 na mshindi wa tatu Miss Kinondoni, Sia Pius, ametamba kwenda kutwaa taji hilo la mlimbwende wa Tanzania kwa mara ya kwanza tangu shindano hilo lirudishwe.

Juzi kati Sia alitembelea Ofisi za New Habari (2006) Ltd, wazalishaji wa magazeti ya Bingwa, Dimba, Mtanzania na Rai kwa ajili ya kutoa shukrani kwa kampuni hiyo ambayo ilidhamini shindano la Miss Sinza 2016, ambalo lilimpa fursa ya kushiriki Miss Kinondoni na hatimaye sasa anaenda Miss Tanzania.

Akiwa katika ofisi za New Habari (2006) Ltd, Sia alifanya mahojiano na gazeti hili na kueleza mengi kuhusu yeye na matarajio yake ya baadaye, mahojiano hayo yalikuwa hivi:-

Bingwa: Unajisikiaje kuibuka mshindi wa kwanza Miss Sinza 2016?

Sia: Kusema ukweli siku ambayo nilitangazwa kuwa mshindi Miss Sinza 2016 nilifurahia sana na siwezi kuisahau kwani niliona ndoto zangu zinatimia.

Bingwa: Ulikuwa na ndoto gani?

Sia: Ndoto ambayo nilikuwa nayo katika maisha yangu kuwa siku nikichukuwa taji la Miss Sinza nitakuwa nimefungua milango ya kuwa mwanamitindo wa kimataifa, nitainua vipaji vya vijana na kuwashauri wasichana wenzangu wenye ndoto kama zangu kupambana kutimiza ndoto zao kwa sababu hakuna kinachoshindikana katika sekta ya urembo, binafsi namshukuru Mungu ni hatua niliyofikia ya kuwa Miss Sinza 2016 na kuwa mshindi wa tatu Miss Kinondoni, lakini safari bado inaendelea ya kuelekea Miss Tanzania.

Bingwa: Umejipangaje na mashindano ya Miss Tanzania 2016?

Sia: Nimejiandaa vema na mashindano ya Miss Tanzania 2016 na nategemea ushindi kwa sababu hakuna kinachoshindikana katika mambo ya urembo na sasa hivi nasubiri kuingia kambini tu hiyo Ijumaa.

Bingwa: Tofauti na mambo ya urembo una kipaji gani?

Sia: Napenda kuwa mtangazaji mkubwa ambaye nitapaza sauti yangu na jamii nzima iisikie katika kutoa elimu juu ya watu ambao wanatumia dawa za kulevya na kutoa elimu masuala ya urembo kwani bado kuna baadhi ya watu hawaelewi urembo na kusema kuwa ni uhuni.

Bingwa: Unapenda kula chakula gani?

Sia: Napenda kula ugali na mboga za majani.

Bingwa: Ni vyakula gani na vinywaji gani ambavyo Miss anatakiwa kula na kunywa?

Sia: Miss unatakiwa kula vyakula vidogo na kama wewe ni mpenzi wa ugali, wali au chakula chochote kula kidogo na kila chakula ambacho unakula ni lazima kula mbogamboga, jitahidi ziwe nyingi, kula matunda mara kwa mara na kwenye vinywaji kunywa maji mengi, maji yanasaidia kutengeneza ngozi na kuondoa mikunjamano ya ngozi mwilini.

Bingwa: Na vyakula gani wanatakiwa wasile mara kwa mara?

Sia: Vyakula ambavyo vina mafuta, najua chakula kikubwa kwa warembo wengi ni chips hiki ni adui wetu namba moja, kwanza chips zinaleta kitambi si chakula cha kula mara kwa mara.

Bingwa: Ni vitu gani ambavyo Miss anatakiwa kufanya mara kwa mara?

Sia: Kufanya mazoezi kwa sana, kujifunza kuongea maneno ambayo kila mtu atatamani kukusikiliza na kuwa na upendo katika mazingira ambayo yanakuzunguka.

Bingwa: Kwenye mwonekano Miss anatakiwa kuwaje suala zima la kuwa tofauti na mtu ambaye si miss kwenye mavazi, usoni, kichwani?

Sia: Miss unatakiwa kuwa tofauti ili mtu akikuona tu  anasema huyu ni Miss, kwanza kwenye uvaaji, unatakiwa kuwa msafi kila saa kila wakati  kuvaa nguo nzuri na yakuvutia ambayo unaweza kuingia sehemu yoyote ile, tukija usoni unatakiwa kuwa makini na vitu ambavyo unapaka usoni na kupata kitu ambavyo vinaendana na ngozi yako na lazima miss kichwani uwe msafi pia kama umesuka suka vitu ambavyo havifichi uso wako na wale ambao wanapenda kuweka mawig pia hakikisha kuwa uso wako unaonekana na yawe marefu.

Bingwa: Kwenye pochi yako kuna vitu gani?

Sia: Kwenye pochi yangu ni lazima niwe na vipodozi, lipstick, pedi, kanga, peni, note book, bond na nguo za kubadilisha.

Bingwa: Kwanini unatembea na nguo kwenye pochi?

Sia: Natembea na nguo za kubadili kwa mfano nipo mbali na eneo ambalo nakaa na nimepata simu ya haraka natakiwa kwenda sehemu kufanya kazi na nguo ambayo nimevaa ni ya kwenda swimming na nguo ya kubadilisha ninayo kwenye pochi, nabadilisha na mambo mengine yanaendelea pia natoa ushauri kwa mamiss kama kwenye pochi zao wajizoeshe kutembea na nguo za kubadilisha.

Bingwa: Kitu gani ambacho kinakubeba na kukufanya watu kukupenda zaidi?

Sia: Silaha yangu katika maisha ni tabasamu, kuwa na furaha wataki wote pia mtu ukiwa na amani na kuwa na tabasamu la kutoka moyoni unaongeza siku ya kuishi.

Bingwa: Unawaambia nini wadau wa ulimbwende na mashabiki zako wategemee nini kutoka kwako?

Sia: Nawapenda sana, wategemee ushindi kutoka kwangu kuwa Miss Tanzania pia sitawaangusha, ombi langu kwa wadau wa ulimbwende na mashabiki zangu ni kuwa na mimi na kama kwenye Miss Tanzania kutakuwa na kupiga kura naomba wanisaidie kunipigia kura kwa wingi ili kunifanikisha kutwaa taji la Miss Tanzania.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Wanaompenda Carlinhos wapewa dili

NA ASHA KIGUNDULA      MASHABIKI na wanachama wa Yanga, wakiwamo wale wanaovutiwa mno na uchezaji...

UKITELEZA KWISHNEI

NA ASHA KIGUNDULAMIAMBA ya soka nchini, Simba na Yanga, leo wana vibarua vigumu vya kusaka pointi zote tatu katika mechi za Ligi...

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na Staa Wako, safu inayokupa nafasi...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -