Tuesday, October 27, 2020

SIAMINI MOURINHO AMEKUBALI TUUONE MWISHO WAKE

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

NA KELVIN LYAMUYA


WAPO binadamu kwa maoni yao, wanasema Jose Mourinho ni mmoja wa makocha bora katika mchezo wa soka duniani. Niwape heshima yao kwa maoni hayo waliyonayo, lakini pia niwape angalizo.

Mourinho huwa hajali maoni kama hayo, ambayo pia ni sifa nzuri kwake. Mourinho anafahamu kwamba, ni watu wachache sana ambao watayakubali. Na si wengi watakaomzungumzia kati ya makocha bora duniani.

Kama ilivyo sasa, wengi wakitaka aondoke Manchester United. Hao wengi pia ni wale wanaoipenda klabu hiyo. Mashabiki wa kutupwa na wengine ambao wanavutiwa na Manchester United.

Binafsi ninadiriki kusema kwamba Mourinho ameweza kusimama imara katika changamoto zote anazokutana nazo Manchester United na inamfafanua katika upande wa kiubinadamu kwamba ni mpambanaji.

Kwa sasa yupo kama mtu aliyekosa wa kuijali nguvukazi yake. Mpaka sasa namwona Mourinho imara ambaye anaamini upo wakati utafika na ataendelea kuwa kocha wa Man United kwa mafanikio.

Historia yake inaonesha kuwa ana wastani wa kukaa kwenye timu moja baada ya mechi 217, kwa hesabu za haraka haraka ni takribani misimu 3.1.

Lakini naamini kuwa Mourinho ataendelea kuwa kocha wa Man United iwapo akisikilizwa na kutimiziwa anachokitaka, kwa kuwa si kocha mbovu bali makosa ya kiubinadamu kwa upande wake na wachezaji ndio yameifanya Man United iwe hivi, kama yeye mwenyewe alivyosema baada ya mchezo wake na Brighton ambao walipoteza kwa mabao 3-2.

Yalikuwa ni matokeo ambayo hayakuwatendea haki Man United kwa wakati huu, kwa sababu Brighton ni moja ya timu ambayo takwimu zake za kufunga mabao haziridhishi mno kwa kiwango cha Ligi Kuu England kabla hata ya kucheza na Man United.

Brighton ilipona kushuka daraja msimu uliopita kwa bahati kubwa mno ya kufanikiwa kukusanya pointi 40 (pointi ambazo zinazoweza kuiokoa timu ya ligi hiyo isishuke daraja).

Lakini ilikuwa ndiyo timu ya nne iliyofunga mabao machache mno kati ya timu sita ambazo zilikuwa hatarini kushuka daraja (pamoja na tatu ambazo hazikuweza kubaki).

Kiufupi Brighton si timu tishio katika kuzitumia nafasi za mabao vyema, dhidi ya Man United walifunga mabao mawili katika jaribio la pili na la tano, ambayo yalikuwa ndiyo mashuti yao ya kwanza yaliyolenga goli.

Takwimu zinaeleza kwamba, katika mechi nyingi za ligi wangefunga bao moja au wasifunge kabisa kutokana na mashuti hayo.

Kosa la kwanza la Man United lilikuwa ni kutojiandaa kikamilifu na hali kama hizo ndani ya uwanja na hilo linatokana na utegemezi wao mkubwa kwa David De Gea akiwa golini, kipa ambaye alisaidia sana kuiokoa timu na kuifanya isipate shida na makosa ya kiubinadamu ambayo yangeifanya timu iadhibiwe na kupoteza mchezo.

La pili, United haikufanya jitihada ili kupata matokeo. Tunafahamu sote kwamba Man United ni timu bora, maana yake ina uwezo wa kupata matokeo bora katika njia yoyote ile hasa ikizingatiwa wana wachezaji wenye vipaji mno lakini baada ya kuwa nyuma mabao matatu, United walipiga mashuti saba tu kabla Paul Pogba hajafunga bao la penalti.

Mourinho sitamlaumu sana, lakini sitaki pia kuamini huu ndio mwisho wake na katika zaidi ya mechi 100 tu ambazo ameiongoza Man United hadi sasa, ndio amekubali tuushuhudie mchana kweupe.

Rekodi zake si mbaya sana, tangu alipoondoka Sir Alex Ferguson ambaye kwa muda mrefu mno aliodumu Man United alikuwa na asilimia 59.67 za kushinda mechi, ni Mourinho mwenye asilimia zinazokaribia na za mzee huyo, 58.25.

Hivyo hata kama hatahitaji kusifiwa na wanaoamini ni kocha bora kama nilivyosema awali, lakini bado ataendelea kuwa mfano bora kwa makocha wengine wanaofuatilia maisha yake ya ukocha hasa kwa jinsi alivyo na uwezo wa kubadilika kuendana na nyakati (najua kuna watu wataipinga hii hoja).

Nguvu kubwa ya Mourinho ni kutotabirika. Leo hii akiisubiri Tottenham Hotspurs, ataingia dimbani na wachezaji wake huku hali ikiwa ni mbaya katika viunga vya Old Trafford.

Lakini bado kocha huyo, pengine ataweza kuibuka na ushindi wa bao 1-0 na anga yote iliyochafuka itageuka kuwa kama mbingu kwa wale wote ambao waligeuka na kumkandamiza, wakitaka aiache klabu ya Manchester United.

Narudia tena, nguvu kubwa ya Mourinho ni kutotabirika, pengine katika miezi ya hivi karibuni, uchovu unaweza kuwa umechukua nafasi kubwa ya kuvuruga amani katika kibarua chake.

Yote yanayoandikwa katika magazeti na kutangazwa kwenye vyombo vya habari si mageni sana.

Kubwa ninalolisubiri ni Mourinho yupi atakayeibuka leo baada ya tabu aliyoipata jana. Huyu naamini atakuwa Mourinho mwenye nguvu kama ilivyo kawaida yake, aliye makini na kazi yake na asiyekata tamaa.

Japokuwa nguvu nazo huwa ni kitu cha kuisha.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -