Tuesday, November 24, 2020

SIKU 90 ZA LWANDAMINA YANGA NA MAJANGA YAKE

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA HUSSEIN OMAR

MWISHONI mwa mwaka jana katika kuhakikisha Yanga inakuwa moto wa kuotea mbali kwenye michuano ya ndani na kimataifa, uongozi wa klabu hiyo uliamua kumleta kocha wa timu ya Zesco United ya Zambia, George Lwandamina, ili kukinoa kikosi hicho.

Yanga ilifikia uamuzi huo baada ya kuona timu yao ikiwa imeshuka kiwango, hivyo kuhofia huenda wakashindwa kutetea taji lao la ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu.

Hatua ya kumleta Lwandamina ilikuja ikiwa ni baada ya Yanga kutoka sare ya 1-1 dhidi ya watani wao Simba katika mtanange wa Oktoba mosi, mwaka jana.

Uongozi wa Wanajangwani hao ulikutana na kutathmini juu ya mwenendo mzima wa kikosi chao, lakini pia wakiyarejea matokeo ya kufungwa bao 1-0 na Stand United mjini Shinyanga katika mechi ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mzambia huyo alianza rasmi kibarua cha kukinoa kikosi cha Yanga, Desemba mosi, akichukua mikoba ya Hans van der Pluijm ambaye alipewa nafasi ya ukurugenzi wa benchi la ufundi kabla ya kutimuliwa.

Katika makala ya haya, BINGWA linakuletea siku 90 alizokaa Mzambia huyo katika kikosi cha Yanga tangu aanze kukinoa.

 

Kupoteza mara mbili dhidi ya Simba

Katika mechi mbili ambazo Lwandamina amekuwa kwenye benchi la ufundi kuikabili Simba, Yanga wameshindwa kupata ushindi.

Mchezo wa kwanza ambao ulikuwa wa michuano ya Kombe la Mapinduzi, Lwandamina alikishuhudia kikosi chake kikipoteza mchezo wa hatua ya nusu fainali baada ya kufungwa kwa mikwaju ya penalti.

Mshindi wa mechi hiyo alilazimika kupatikana kwa penalti baada ya timu hizo kongwe kutoka sare ya 0-0 dakika zote 90 za kipute hicho.

Mchezo wa pili kuishuhudia Yanga ikipoteza mbele ya Simba huku Lwandamina akiwa kwenye benchi la ufundi la Yanga, ni ule wa wiki chache zilizopita uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa.

Katika mtanange huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga ya Lwandamina iliambulia kichapo cha mabao 2-1 na kushuhudia Simba wakiondoka na pointi tatu wakiwa pungufu.

 

 

Kufungwa na Azam

Katika kile kinachoakisi ugumu wa Yanga ya sasa kuhimili vishindo vya timu kubwa, tayari imeshapoteza mchezo mmoja dhidi ya Azam.

Mtanange huo ulikuwa wa hatua ya robo fainali ya Kombe la Mapinduzi uliochezwa Visiwani Zanzibar ambapo Azam ilitwaa ubingwa wa michuano hiyo.

Ikumbukwe kuwa Lwandamina hakuwa amefika wakati Yanga ilipoambulia sare ya 0-0 katika mchezo wa mzunguko wa kwanza dhidi ya Azam ambao ulikuwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

 

Kufeli kwa Zullu

Usajili wake ulikuwa wa mbwembwe nyingi hasa kutoka kwa mashabiki wa Yanga ambao walimpachika jina la ‘Mkata Umeme’.

Lwandamina alimsajili nyota huyo kutokana na kiwango kizuri alichokionesha wakati walipokuwa pamoja katika klabu ya Zesco.

Lwandamina aliamua na kuwaaminisha viongozi na mashabiki wa Yanga kuwa Zullu ni hatari katika suala zima la ukabaji tatizo ambalo linaikabili timu hiyo kwa muda mrefu sasa tangu kuondoka kwa kizazi cha akina Athumani Idd ‘Chuji’.

Presha na taarifa za ujio wa Zullu ndiyo iliyosababisha baadhi ya mashabiki wa Yanga kuanza kumdharau Twitte na kumwita ‘babu’.

Lakini je, kazi anayoifanya Zullu katika safu ya kiungo wa ulinzi pale Yanga imefikia japo nusu ya Twitte?

Zullu ni mzito kupandisha mashabulizi licha ya uwezo wake mzuri wa kupiga pasi ndefu, lakini pia si mzuri katika kuzuia mashambulizi (kukaba) pindi timu inapozidiwa.

Kwa aina ya uchezaji wake wa taratibu ni rahisi kumwona akichemsha pindi anapocheza dhidi ya viungo wepesi kama Jonas Mkude, Mohamed Ibrahim na Said Ndemla wote wa Simba na wengine kama Salum Abubakari ‘Sure Boy’.

Ni wazi kuwa Yanga wanapaswa kujiuliza mara mbili juu ya hatima yao kwenye safu ya kiungo wa ulinzi ila kwa Zullu wamechemsha.

 

 

 

Nidhamu mbovu kwa wachezaji

Hivi karibuni mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe, Dornald Ngoma, alitajwa kususia mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya mahasimu wao Simba.

Baada ya Haroun Ali kuthibitisha kuwa Ngoma alikuwa fiti kwa asilimia 100 kucheza mchezo huo, straika huyo alipingana na taarifa hiyo ya kitaalamu na kusema hajapona, hivyo asingeweza kuingia uwanjani.

Mbali na kitendo hicho cha utovu wa nidhamu, pia beki kisiki na nahodha wa Wanajangwani, Vicent Bossou, aligomea kucheza mechi hiyo.

Inaelezwa kuwa sababu ya nyota huyo raia wa Togo kufikia uamuzi huo ni kitendo cha mabosi wa Yanga kushindwa kumlipa mishahara yake ya miezi mitatu.

 

Kushindwa kupandisha viwango vya wachezaji

Wakati anachukua mikoba ya Pluijm kukinoa kikosi cha Yanga, Mzambia huyo alikuta baadhi ya wachezaji viwango vyao vikiwa chini kwa namna moja au nyingine alikuwa na kazi ya ziada kuhakikisha anapandisha viwango vya nyota hao.

Lakini katika siku 90 Lwandamina alizokaa Yanga na kufundisha ameonyesha kushindwa kupandisha viwango vya wachezaji kama Athony Matheo, Geofrey Mwashiuya, Pato Ngonyani, Said Juma ‘Makapu’ Malimi Busungu na Yusuph Mhilu.

 

 

Timu haichezi soka la kuvutia

Katika mechi za hivi karibuni, Yanga wamejikuta wakianza vizuri dakika 15 hadi 20 za mwanzo, ambapo wamekuwa wakionekana kuwa na kasi ya hali ya juu, lakini morali yao hushuka kadiri muda unavyozidi kwenda.

Mfano mzuri ni mchezo wao wa hivi karibuni dhidi ya Simba ambapo walianza mchezo kwa kasi na kuwakamata vizuri wapinzani wao hao katika muda huo na hatimaye kupata penalti iliyofungwa na Simon Msuva.

 

Siasa

Ni ngumu kwa Lwandamina kufanikiwa akiwa Bongo ikiwa hakujipanga mapema kukabiliana na siasa zilizojaa katika mchezo wa soka hapa nchini. Hivi sasa zimeanza kumwathiri kwa kiwango kikubwa.

Kwanza, kuelekea mchezo wake dhidi ya Simba, suala la kambi lilianza kupigwa danadana kiasi kwamba huenda iliwavuruga kisaikolojia wachezaji wa kikosi hicho.

Awali, kulikuwa na taarifa kuwa timu hiyo ingekimbilia Visiwani Zanzibar kujiandaa na mchezo wao dhidi ya wapinzani wao Simba lakini baadaye walikurupuka ghafla na kwenda Kimbiji. Ni wazi kabisa kuwa wachezaji na benchi la ufundi hawakuwa na utulivu wa kutosha kuelekea mtanange huo.

Lakini pia, hivi  sasa kuna mvutano kati ya uongozi wa Yanga na wachezaji Bossou na Ngoma. Wakati viongozi wakikanusha taarifa hizo, mastaa hao wa kigeni wanadai kutolipwa mishahara yao. Hizo ndizo siasa ambazo zimeanza kumkuta Lwandamina.

 

Lwandamina ni nani?

Beki huyu wa zamani wa Mufurila Wanderers na timu ya taifa ya Zambia, alizaliwa Agosti 5, 1963 na kustaafu kucheza soka mwaka 1995 kutokana na majeraha ya goti yaliyomsumbua kwa kipindi cha miaka mitatu.

Mwaka 2014 aliteuliwa rasmi kuwa kocha mkuu wa Zesco United na kufanikiwa kutwaa mataji mawili ya ndani katika msimu wake wa kwanza.

Pia Lwandamina alifanikiwa kubeba tuzo ya kocha bora wa Zambia mara mbili mfululizo, mwaka 2014 na 2015.

Akiwa na Zesco, Lwandamina anajivunia rekodi ya kuiongoza klabu hiyo kucheza hatua ya nusu fainali Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka huu akivuka kwenye kundi la kifo.

Zesco walipangwa Kundi A sambamba na Wydad Casablanca ya Morocco, Al Ahly ya Misri na Asec Mimosas ya Ivory Coast, walimaliza wakiwa na pointi tisa na kushika nafasi ya pili nyuma ya timu ya Morocco.

Dhidi ya Al Ahly ambao wamekuwa wakiisumbua sana Yanga kila wanapokutana, Lwandamina aliiongoza Zesco kupata pointi nne, wakishinda 3-2 mchezo wa kwanza nyumbani na kulazimisha sare ya bao 2-2 ugenini.

 

Timu ya taifa

Lwandamina aliyepata mafunzo ya ukocha nchini Ujerumani na Uholanzi, alianza kukinoa kikosi cha vijana wa Zambia U-20 mwaka 2003 hadi 2008 na kufanikiwa kutwaa Kombe la Cosafa.

Mwaka 2007, aliingoza timu hiyo kucheza nusu fainali ya Kombe la Afrika kwa vijana na kupata tiketi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia la vijana yaliyofanyika Canada, ambapo Zambia waliishia hatua ya 16 bora.

Mwaka 2005 aliteuliwa kuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Zambia chini ya Kalusha Bwalya, akichukua nafasi ya kocha wa zamani wa Simba, Patrick Phiri.

Lwandamina aliendelea na kazi hiyo chini ya Hervé Renard aliyechukua nafasi ya Kalusha.

Mwaka 2010 baada ya Renard kubwaga manyanga, Lwandamina alipewa kwa muda kuiongoza Zambia kwenye michezo miwili ambayo alipoteza yote na kunyimwa kibarua hicho.

Lakini hii haikuwa mwisho wa safari yake na timu ya taifa ya Zambia ambapo Mei 2015, siku tano kabla ya pambano la kufuzu fainali za Afrika dhidi ya Guinea-Bissau, Lwandamina alipewa jukumu la ukocha mkuu wa taifa hilo.

Akiwa kocha mkuu Lwandamina aliiongoza Zambia kufuzu fainali za Afrika 2016 ambapo walitolewa kwenye hatua ya mtoano na Guinea kwa changamoto ya mikwaju ya penalti.

Ikumbukwe Wanajangwani hao walimtimua kocha Ernest Brandts na benchi zima la ufundi baada ya kipigo cha mbao 3-1 dhidi ya Simba katika mchezo maalumu wa kirafiki maarufu Nani Mtani Jembe uliochezwa  Uwanja wa Taifa, Desemba mwaka 2013.

Yanga ilifanya hivyo tena kwa mwaka uliofuata kwa Mbrazil, Marcio Maximo, baada ya kufungwa 2-0 na Simba katika mechi ya Mtani Jembe iliyochezwa Desemba 13, 2014 na mikoba yake kuchukuliwa na Pluijm.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -