Friday, November 27, 2020

Siku ya Msanii ilifana ila wasanii wenye majina walitia aibu

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA CHRISTOPHER MSEKENA

MAZOEA ni mabaya, hasa unapozoea kutenda jambo baya na nafsi yako ikakataa kabisa kuliacha jambo hilo linalokupa furaha binafsi licha ya kutoa kero kwa watu wengine.

Huwezi kuona tatizo mpaka pale utakapopata madhara ndiyo utashtuka na kuona jambo hilo ulilokuwa unalifanya kwa mazoea ni baya na hukupaswa kuliendekeza.

Mfano mdogo ni hili la Bongo Fleva. Mpaka leo hii hakuna muziki wa Tanzania unaoweza kusimama kama ulivyosimama muziki wa Kwaito kutoka Afrika Kusini na ule muziki ulioletwa na wasanii kutoka Nigeria.

Ladha kutoka Bongo au Bongo Fleva kama inavyoitwa ni muziki wenye umri unaokadiriwa miaka 15, lakini makuzi yake yamechangiwa zaidi na aina za muziki kutoka mataifa mengine kama vile Marekani, Ulaya na baadhi ya nchi za Afrika.

Asilimia 90 ya miziki iliyounda Bongo Fleva ni sampo kutoka kwenye mataifa mbalimbali na asilimia 10 ndiyo miziki ya kwetu inayotukutanisha na wasanii kama Mrisho Mpoto, Saida Karoli na wengine wanaoimba muziki wa asili.

Asilimia 10 ni ndogo mno kuleta ushindani mbele ya Kwaito inayosikilizwa na watu wengi zaidi Afrika na hapo sasa ndiyo tunaona mazoea ya kusampo miziki ya watu inavyotutoa jasho kutafuta muziki utakaoitambulisha Tanzania.

Mazoea ni yale ya kusampo RnB na hip hop ya Marekani na kuileta kwenye mazingira yetu, kiasi kwamba hizo sampo zimeupoteza kabisa muziki wetu wa asili na sasa tunatoa jasho kuisimamisha singeli ambayo nayo tumesampo kwa wale makapuku wa Misri walioutumia muziki huo enzi wanadai usawa kwa matajiri wa nchi hiyo.

Mazoea ndiyo yameifikisha hapa Bongo Fleva yenye wasanii wanaofanya muziki kwa kudukua aina mbalimbali za muziki unaofanywa na mataifa mengine na kukuletea wewe shabiki ambaye licha ya nyimbo hizo kudukuliwa, umeendelea kuusapoti na kuwaunga mkono wasanii wake.

Mazoea ya kusampo yamewapa wasanii mafanikio kifedha. Sampo ndiyo zimetuletea wasanii wakali tulionao sasa, tunaachaje kuendelea kusampo wakati kuna faida nyingi na hasara inabaki kwa taifa linapokosa muziki wenye utambulisho wake.

Mazoea hayo hayo tunayapeleka kwenye mambo ya msingi kwa ustawi wa sanaa yetu. Mashabiki wanaunga mkono harakati za wadau kustawisha sanaa ila wasanii wenyewe hawataki. Wanajivunia ukubwa wa majina yao, hawataki kabisa kuchangamana na wasanii wa sanaa nyingine, wamekumbatia umaarufu licha ya umaarufu wao kujengwa na muziki wa sampo.

Hawapendi kabisa kusikia habari ya matamasha, makongamano au semina zinazotoa elimu kuhusu sanaa. Hawataki kuongeza maarifa na kujifunza mambo mapya kutoka kwa watu wanaoijua vyema sanaa, wanajiona wapo sahihi ilhali kazi zao zina makosa mengi ambayo ni kero kwa sisi mashabiki.

Leo hii tunaletewa Siku ya Msanii, siku inayoikumbusha jamii uwepo wa wasanii ndani ya nchi yao, ila jambo la ajabu na la kutia aibu kwa mtu anayefahamu umuhimu wa siku hii, wasanii ambao ndiyo wahusika hawatokei eneo la tukio.

Hii ni siku ambayo wasanii wa sanaa mbalimbali hukutana na kuonyesha kazi zao za sanaa kwa mashabiki. Hii ndiyo siku ambayo msanii wa sanaa moja anaweza kuongeza maarifa kupitia kazi za msanii mwingine, ila hali haikuwa hivyo.

Tuliohudhuria tamasha lile tulijionea utamu wa sanaa zetu nje ya Bongo Fleva na filamu. Macho na mioyo yetu iliburudika na sanaa za maonyesho pamoja na sanaa za ufundi, tukajifunza kumbe kuna utajiri mkubwa ndani ya sanaa hizo zilizokosa mashiko mbele ya kizazi kipya.

Wasanii wakubwa wenye majina hawakuja licha ya kupewa mialiko, mazoea yao wameyaleta kwenye mambo ya msingi, wamekosa elimu iliyojaa maarifa ya kustawisha muziki na filamu zao.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -