Saturday, January 16, 2021

SIMBA AKILI YOTE KWA JKT RUVU

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA SALMA MPELI

SIMBA wanajua ugumu wanaoupata kuwafunga JKT Ruvu katika mechi zao za Ligi Kuu Tanzania Bara na sasa kocha mkuu wa timu hiyo, Joseph Omog, amepata mbinu kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo wao wa kesho dhidi ya maafande hao.

Wekundu wa Msimbazi wanajua shughuli ya JKT Ruvu ambayo walishindwa kuifunga katika raundi ya kwanza na wanafahamu kwamba kama watapoteza mchezo huo watakuwa wametoa mwanya mkubwa kwa mahasimu wao, Yanga katika mbio za ubingwa kuwafikia na kuwapita.

JKT Ruvu ni moja ya timu ambazo zinaisumbua Simba, hasa baada ya kuwalazimisha sare na pia kuwafunga katika baadhi ya mechi muhimu.

Hata hivyo, tayari Simba wamepanga mikakati ya kuhakikisha hawapotezi kwa JKT Ruvu, kwani wakiruhusu bao wanaweza kuharibu rekodi yao ambayo wameiweka msimu huu ya kuendelea kuongoza ligi hiyo kutokana na pointi 38 wakifuatiwa na Yanga wenye pointi 36.

Kocha Omog anatarajiwa kuwatumia wachezaji wake wote waliosajiliwa wakiwamo wa kigeni baada ya kukamilisha vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini.

Simba na klabu nyingine zilizosajili wachezaji wa kigeni walizuiliwa kucheza na Idara ya Uhamiaji, baada ya kubainika kwamba walikuwa hawana vibali vya kuishi na kufanya kazi nchini.

Kwa mujibu wa Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’, wachezaji wote wa kigeni na makocha wao ambao walikuwa hawana vibali ni ruksa kucheza baada ya kukamilisha utaratibu wa kuwaombea vibali katika Wizara ya Kazi.

Kaburu alisema vibali vya wachezaji wao; Javier Bokungu, Laudit Mavugo, Fridrick Blagnon, Method Mwanjale,  James Kotei, Daniel Agyei, vilikamilika tangu juzi na jana walikamilisha vya makocha wao, Omog, Jackson Mayanja raia wa Uganda  na Abdul Idd Salum (Kenya).

Akizungumza na BINGWA jana, Omog alisema kutokana na ugumu wa mechi hiyo wamejipanga vizuri baada ya kufanya maboresho kwa kiwango kikubwa katika kikosi chake.

Omog alisema wanahitaji kushinda ili waweze kuendelea kukaa kileleni na baadaye kuchukua ubingwa wa msimu huu, baada ya kuukosa kwa misimu minne mfululizo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -