Saturday, October 31, 2020

SIMBA, AZAM FC ZAPEWA WAKUBWA FA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA WIFRIDA MTOI

RATIBA ya Kombe la Shirikisho nchini (FA) hatua ya 16 bora imetoka, ambapo Simba na Azam zimeangukia kwa timu vigogo, huku Yanga ikionekana kupata mteremko baada ya kupewa Kiluvya United inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.

Katika ratiba hiyo iliyotolewa jana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), inaonyesha Simba watachuana na African Lyon Machi mosi katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, huku Azam wakiangukia kwa Mtibwa Sugar watakayokutana nayo Februari 24 katika Uwanja wa Azam Complex.

Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa kombe hilo, watacheza na Kiluvya Machi 7, mwaka huu katika dimba la Taifa, timu ambayo ilitinga nafasi hiyo baada ya kuwatoa Ruvu Shooting.

Simba wanakutana na Lyon wakiwa na kumbukumbu ya kupokea kipigo cha bao 1-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara katika  mzunguko wa kwanza.

Katika hatua nyingine, Kagera Sugar itakutana na Stand United kwenye  Uwanja wa Kaitaba Februari  24, Might Elephant dhidi ya Ndanda FC, Uwanja wa Majimaji Songea, Madini FC itakuwa katika Uwanja wa Sheikh Abeid, Arusha ikiwaalika Mafaande wa JKT Ruvu siku hiyo.

Michezo mingine itapigwa Februari 26, Mbao FC itaumana na Toto Africans kwenye  Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, wakati  Mbeya City itapepetana na  Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine Mbeya.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -