Monday, January 18, 2021

SIMBA HAITAKAGI UJINGA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA JUMANNE JUMA, MTWARA

SIMBA haitakagi ujinga. Hivyo ndivyo unavyoweza kusema. Vinara hao wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara, jana wamerejea kileleni kwa kuilaza Ndanda FC ya Mtwara mabao 2-0.

Mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara, ulishuhudia Simba ikilazimishwa kwenda mapumziko bila kufungana.

Muzamiru Yassin na Mohamed Ibrahim ‘Mo’, walipeleka kilio kwa wenyeji Ndanda na kuwafanya warejee kwenye kiti chao ambacho mahasimu wao, Yanga wakilikalia kwa saa 24 tu baada ya wao juzi kuilaza JKT Ruvu mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

Kwa matokeo hayo, Simba wamefanikiwa kufikisha pointi 38 wakifuatiwa na Yanga wenye pointi 36 baada ya kila timu kucheza mechi 16.

Ndanda walikuwa wa kwanza kufanya shambulio langoni mwa Simba baada ya Hamis Rifat kupiga shuti kali dakika ya kwanza, lakini halikulenga lango.

Baadaye Ndanda walifanya shambulizi lingine dakika ya pili, baada ya beki wa timu hiyo, Paul Ngalema, kupanda na mpira na kupiga shuti kali, lakini kipa wa Simba, Daniel Agyei, alidaka.

Simba walijibu mapigo dakika ya tatu, baada ya Shiza Kichuya kupiga krosi safi, lakini Fredrick Blagnon alishindwa kumalizia.

Ndanda walioonekana kutawala mchezo walipoteza nafasi nyingine ya kufunga, baada ya Kigi Makasi kuingiza krosi nzuri lakini iliishia mikononi mwa Agyei.

Hata hivyo, mpira ulisimama dakika ya 13, baada ya kiungo wa Simba, James Kotei, kugongwa kiwiko wakati wakiwania mpira na Makasi.

Simba walifanya mabadiliko dakika ya 15, baada ya Kotei kuonekana ameumia na nafasi yake kuchukuliwa na kiungo mwenzake, Muzamiru.

Dakika ya 22, Ndanda walifanya shambulizi kali lakini beki wa Simba, Javier Bokungu aliondoa hatari hiyo kwa kutoa mpira nje na kuwa kona tasa.

Ndanda ambao walionekana kulishambulia lango la Simba mara kwa mara, walipoteza nafasi nyingine dakika ya 24, baada ya Omar Mponda kupiga shuti kali lakini Agyei alidaka.

Ibrahim Ajib almanusura aifungie Simba bao dakika ya 27, lakini shuti lake lilimbabatiza beki wa Ndanda na kuokolewa.

Simba walionekana kuamka dakika ya 35, lakini mashambulizi yao yalizimwa na mabeki wa Ndanda ambao walionekana kuwa makini wakati wote.

Katika dakika ya 40, Simba walipata nafasi nzuri ya kufunga na Ibrahim kupiga shuti kali ambalo halikuwa na madhara.

Simba waliingia kipindi cha pili kwa kasi mpya na kufanikiwa kupata kona dakika ya 52, lakini haikuzaa matunda baada ya mabeki wa Ndanda kuokoa.

Ibrahim akiwa katika nafasi nzuri alishindwa kufunga baada ya kuingia na mpira huku Kichuya akipiga shuti hafifu ambalo liliishia kwa kipa wa Ndanda.

Muzamiru alifunga bao la kwanza kwa Simba dakika ya 63, baada ya kupiga shuti kali ndani ya eneo la 18 kutokana na kazi nzuri aliyoifanya Ibrahim.

Bao hilo liliongeza ari kwa Simba, ambapo dakika ya 81, Ibrahimu aliongeza la pili aliyefunga kwa shuti kali.

Kabla ya kufunga bao hilo, Simba walifanya shambulizi dakika ya 78, lakini Kichuya alishindwa kufunga, baada ya kupiga shuti lililoondolewa katika eneo la hatari na mabeki wa Ndanda.

Katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Zainab Iddy, anaripoti kuwa African Lyon walitoka sare tasa na Azam, wakati Mbao wakiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Stand United kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Kutoka Uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya wenyeji, Tanzania Prisons waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Majimaji, ambapo bao pekee katika mchezo huo, lilifungwa na Victor Hangaya dakika ya 59.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -