Friday, October 23, 2020

SIMBA HII NI MABAO TU *Mbelgiji aja na mbinu zitakazozidi kuwapa heshima Okwi, Kagere, Kichuya

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA HUSSEIN OMAR

UNAWEZA kudhani siku tatu zilizobaki kabla ya Simba kukipiga na Stand United katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ni nyingi, lakini kwa kocha mkuu wa timu hiyo, Mbelgiji Patrick Aussems, ni chache mno, hivyo amekuja na mbinu mpya za upatikanaji wa mabao.

Akifahamu ubora wa washambuliaji wake, Mbelgiji huyo anaonekana kutoridhishwa na idadi ya mabao wanayofunga, hivyo kuamua kulifungia kazi suala zima la uchekaji na nyavu, huku lengo likiwa si chini ya mabao matatu kila mechi ili kuwa katika mazingira mazuri ya kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

 

Safu ya ushambuliaji ya Simba inayoongozwa na Emmanuel Okwi mwenye bao moja na Meddie Kagere aliyefikisha manne, imejikusanyia mabao nane ndani ya michezo saba ya Ligi Kuu Bara.

Na kinachowaumiza zaidi Wekundu wa Msimbazi hao, ni kasi ya wapinzani wao, Yanga na Azam, hivyo Mbelgiji huyo ameona ni vema kuja na mkakati mpya ambao amekuwa akiufanyia kazi mazoezini ili timu hiyo iweze kutisha.

Kwenye mazoezi yaliyofanyika juzi na jana kwenye Uwanja wa Boko Veterans, BINGWA lilishuhudia Aussems akiwataka wachezaji wake kutumia sekunde 10 tu kushambulia na kurudi kukaba.

Katika zoezi hilo, Aussems aliwataka wachezaji wake kupiga pasi tatu tu zitakazowawezesha kufika golini kufanya shambulizi na kurejea kukaba.

Aussems alionekana kuwatumia mawinga; Shiza Kichuya, Asante Kwasi, upande wa kushoto kupiga krosi, huku upande wa kulia, Rashid Juma, Mohammed Ibrahim na Said Ndemla, wakitakiwa kuhakikisha krosi zao zinawafikia washambuliaji; Adam Salamba, Marcel Kaheza na Mohammed Rashid.

Iwapo mfumo huo utafanikiwa unaweza kuwasaidia washambuliaji wa Simba; Okwi, Kagere na John Bocco, kufunga mabao mengi zaidi.

Baada ya mazoezi hayo kumalizika, Aussems, alisema takribani wiki ya pili amekuwa na kazi ya kuhakikisha washambuliaji wake wanakuwa wepesi kwa kupachika mabao.

Alisema kikosi cha Simba ni kipana kina wachezaji wazuri ambao wanahitaji kupata muda zaidi ili waweze kuendana na falsafa yake.

“Bado siridhishwi na upatikanaji mabao, ninahitaji kuwajenga zaidi wachezaji wangu kuweza kupata mabao mengi, nina kikosi bora ambacho naamini kinaweza kufanya jambo lolote uwanjani,” alisema Aussems.

Matokeo hayo yameifanya Simba kufikisha pointi 14 na kupaa hadi nafasi ya nne kutoka ya tisa waliyokuwapo awali.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -