Saturday, January 16, 2021

SIMBA ILIAMINI KATIKA MATOKEO, YANGA ILIAMINI KATIKA MCHEZO IKASAKA MATOKEO

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

DAKIKA 90 za mchezo Simba dhidi ya Yanga miaka nenda rudi maandalizi yake yamekuwa na tofauti kubwa na maandalizi ya mechi zingine wakati timu hizo zinapokutana na timu nyingine. Aliyejificha Pemba ataisifia kambi yake imetiki na juma zima hili utasikia kila aina ya mbwembwe na dhihaka dhidi ya yule aliyejificha Unguja.

Mchezo wa soka mara zote huambatana na burudani ambayo inatokana na kiwango halisi na umahiri wa usakataji wa soka kutoka kwa wachezaji uwanjani. Uhalisia wa mchezo ukiachana na matokeo ya ushindi kwa upande wa Yanga, bado kuna mapungufu kiasi chake katika uwajibikaji kutokana na ukubwa wa majina ya timu hizi zenye mashabiki wengi na timu ambazo ni kongwe katika historia ya soka la Tanzania.

Kadi za njano zaidi ya kumi na nyekundu moja inakupa picha halisi ya ladha gani ya soka watazamaji tuliikosa kutoka dimbani. Dakika 45 za kipindi cha kwanza Simba walicheza ili kuonyesha jukwaa kuwa wao wana uwezo mkubwa wa kumiliki mpira na kutengeneza nafasi kuliko upande wa pili wa Yanga ambao walionekana kuingia kinyonge.

Kwa kuwa mpira wa mguu matokeo ndiyo kila kitu, mbinu za ufundi zinachukua nafasi yake, weledi na jicho la taaluma na busara za kocha katika kufanya maamuzi pia ni jambo lingine la msingi. Hapa ndipo unapoanza kumtofautisha na kiongozi kama mtawala pamoja na shabiki. Kocha wa Yanga, Hans Van Pluijm, alifanya uamuzi wa kiufundi mno pale alipoamua kumtoa Simon Msuva kwa kushindwa kutimiza majukumu yake aliyomtuma na kumuingiza Malimi Busungu, baada ya dakika 35 tu za mchezo na dakika saba baadaye mabadiliko hayo yakazaa matunda.

Mabadiliko yaliipa ari, bao la Amissi Tambwe lilitokana na mpira wa mashambulizi ukianzia kwa Busungu, huyu Busungu ambaye inawezekana aliingia uwanjani akiwa na mambo matatu, kwanza kutimiza maelekezo ya mwili, pili huenda jicho lake lilisoma bango la shabiki wa timu yake lililosomeka ‘Mungu si wa upande mmoja’ na mwisho pengine alikuwa na siri ya ule ukimya wa viongozi wa timu yake katika kipindi chote cha maandalizi dhidi ya mahasimu wao.

Vitu hivi vikampa chachu ya kumaliza mchezo kwa kupachika bao la pili kwa kutumia udhaifu wa beki wa kulia wa Simba, Ramdhani Kessy kwa kupiga mpira wa kichwa mbele yake. Hizi ndizo mbinu za makocha kupata matokeo katika mchezo mgumu, kocha anawasoma wachezaji wakati mchezo ukiendelea na haraka anatumia udhaifu wa adui kupata matokeo.

Haimaanishi kwamba, Dylan Kerr, kocha wa Simba ni mbaya au aliishiwa mbinu za ushindi, hapana huenda majukumu aliyowatuma wachezaji wake hawakutimiza ipasavyo, kilichoonekana tangu mwanzo hata lugha ya mwili ikisomeka kutoka kwa wachezaji ni kujiamini kupitiliza. Kwa kuwa na matokeo mazuri ya siku za usoni dhidi ya Yanga na hata matokeo ya mwanzo wa ligi yaliwapa hisia za kuendelea kuwa watawala bila kufikiria kwamba wapinzani wao walikuwa na hasira mno wa kufuta uteja.

Kwa ufupi unaweza tu kusema madhara ya kujiamini kupitiliza kwa wachezaji wa Simba na kusahau kabisa kama rekodi zipo ili zivunjwe, kuliwagharibu kuwapa adhabu ya kupoteza mchezo huo. Pia hawakutaka kujikumbusha kama bado wana mlima mrefu mbele ya Mtani wake huyo, kupunguza idadi ya mechi nyingi za kufungwa na mtani wake. Kujiamini ni muhimu lakini inatakiwa kujiamini kimchezo na si kujiamini kimatokeo. Simba ilijiamini kimatokeo na waliona kwa namna yoyote ile watashinda, Yanga walijiamini kimchezo na walikuwa wakisaka matokeo na wakayapata.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -