Saturday, October 31, 2020

SIMBA ILISHINDWA KULIPA KISASI KWA YANGA 1996

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA HENRY PAUL

TIMU ya Simba ilishindwa kulipiza kisasi cha kufungwa na Yanga, baada ya kulazimishwa kutoka sare ya bao 1-1, katika mchezo wa marudiano ya Kombe la Hedex, uliofanyika mwaka 1996, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam (sasa Uwanja wa Uhuru).

Katika mchezo wa kwanza baina ya timu hizo, uliochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, mjini Mwanza wiki mbili nyuma, Yanga iliifunga Simba mabao 2-0. Hivyo kwa matokeo hayo, Yanga iliitoa Simba katika michuano hiyo kwa jumla ya mabao 3-1.

Kwa ushindi huo Yanga, ilizawadiwa hundi ya shilingi milioni 3.5 na wadhamini wa michuano hiyo, Kampuni ya Golden Marketing ya Kenya, huku Simba wakiambulia shilingi milioni 1.5.

Wachezaji wa Yanga, pia walitunukiwa medali na mgeni rasmi, aliyekuwa Mkuu wa Polisi nchini, Omari Mahita.

Matokeo hayo yalizima kabisa jitihada za Simba kupania kulipiza kisasi kwa Yanga ambayo iliwazuia wachezaji wake wanne waliokuwa timu ya Taifa Stars kwenda Malawi na timu hiyo kwa mwaliko wa mechi za kirafiki ili kujiandaa na mchezo huo.

Wakati huo huo kuonesha matunda, Yanga iliamua kupeleka wachezaji wake 14 kwa timu hiyo ya Taifa Stars iliyokuwa imekwenda Malawi.

Mchezo huo ulianza kwa kasi kwa timu zote kushambuliana kwa zamu na katika dakika tatu za mwanzo beki wa Simba, George Masatu, kipa wa Yanga, Joseph Katuba, walilazimika kufanya kazi ya ziada kuokoa hatari katika milango yao.

Dakika nne baadaye mshambuliaji, Mohamed Hussein wa Yanga, alimpokonya mpira beki wa Simba, Alfonce Modest, karibu na lango, lakini alipiga shuti hafifu lililokuwa ‘mboga’ kwa kipa wa Simba, Stephen Nemes.

Baada ya kosakosa hiyo uliwadia wakati wa furaha kwa mashabiki wa Simba ambao hawakuonekana kuwa na furaha tokea walipoingia uwanjani.

Furaha hiyo ilitokana na bao lililofungwa na Hussein Marsha kwa penalti katika dakika ya 25 kufuatia beki wa Yanga, Kenneth Mkapa, kuunawa mpira wakati yeye, Abdallah Msheli na Rouben Mgaza, walipokuwa wakijaribu kumdhibiti, Ally Yusuf ‘Tigana’, aliyekuwa akiwapangua ili akaonane ana kwa ana na kipa Katuba.

Yanga washangiliaji wake maalumu wa matarumbeta waliingia na kurusha njiwa wawili uwanjani na mmoja alielekea goli lililoko Kusini mwa Uwanja wa Taifa alikoweka ‘maskani’ ya muda kabla ya kutimuliwa na shabiki wa Simba.

Jitihada za vijana wa Mtaa wa Jangwani na Twiga kutaka kuwadhihirishia wana Simba kwamba hawana masihara mwaka huo, zilifanikiwa kuzaa matunda katika dakika ya 33, wakati beki wa timu hiyo, Bakari Malima, alipoirudia staili ya bao aliloifungia timu yake mjini Mwanza kwa kupachika wavuni bao la kusawazisha.

Bao hilo alilolifunga kwa kichwa lilitokana na kona murua iliyochongwa na winga machachari wa timu hiyo, Edibily Lunyamila ambaye kwa furaha aliamua kuivua jezi yake na kuipunga hewani kabla ya kuivaa tena na kuendelea na mchezo.

Dakika tatu baadaye Yanga nusura ipate bao la pili wakati Lunyamila alipomtangulizia mpira Mohamed Hussein golini mwa Simba, huku kipa Stephen Nemes akiwa ameshatoka katika lango lake.

Lakini mpira alioupiga ulitolewa nje na Hussein Marsha. Hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika timu zilikwenda mapumziko matokeo yakiwa ni sare ya bao 1-1.

Kipindi cha pili kiliendelea kuwa na kasi na Yanga walifanya shambulizi la nguvu katika lango la Simba, lakini kiungo mshambuliaji, Yusuf Macho, aliyekuwa amebaki peke yake na nyavu baada ya kunyunyiziwa majalo na winga wa kulia Sanifu Lazaro, alipiga mpira nje.

Simba walijibu shambulizi hilo katika dakika ya 75 ya kipindi cha pili, wakati beki Deo Mkuki, alipomtangulizia mpira Alfonce Modest, aliyekuwa amekwenda mbele kusaidia mashambulizi, lakini alipiga kiki kali iliyotoka sentimita chache ya lango la Yanga.

Katika mchezo huo wachezaji; George Masatu, Abdallah Msheli, Joseph Katuba, Stephen Nemes na Sanifu Lazaro, walioneshwa kadi za njano na mwamuzi, Bakari Mtangi kutoka Tanga kwa makosa mbalimbali.

Kikosi cha Simba kiliwakilishwa na kipa Stephen Nemes, Deo Mkuki, Alfonce Modest, Mustapha Hoza/Shabani Ramadhani, George Masatu, Hussein Marsha, Akida Makunda/Thomas Kipese ‘Uncle Thom’, Athumani China, Bita John/Edward Chumila (marehemu) na Dua Said.

Kikosi cha Yanga kiliwakilishwa na kipa Joseph Katuba (marehemu), Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’, Kenneth Mkapa, Rouben Mgaza, Abdallah Msheli/Thabit Bushako, Salvatory Edward, Sekiojo Chambua/Sanifu Lazaro ‘Tingisha’, Yusuf Macho ‘Musso’, Said Mwamba ‘Kizota (marehemu), Mohamed Hussein ‘Mmachinga’ na Edibily Lunyamila.

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -