Saturday, November 28, 2020

SIMBA INAKAMUA TU KAMA KAWA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAINAB IDDY


SIMBA inakamua tu kama kawa baada ya jana kuendeleza wimbi la ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Alex Mahagi kutoka Mwanza, Simba walipata bao pekee kupitia kwa Mohamed Ibrahim.

Kwa matokeo hayo, Simba wamefanikiwa kufikisha pointi 44 wakiendelea kukimbizana kileleni na Yanga ambao wanawafuatia nyuma kwa pointi 40, baada ya juzi kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Ndanda.

Simba walianza mchezo kwa kasi kwa lengo la kupata bao la mapema, lakini mabeki wa Ruvu Shooting walionekana kuwa makini kuondoa mashambulizi.

Washambuliaji wa Simba walifanya mashambulizi dakika ya 13, 24, 27 na 34, lakini Shiza Kichuya na Mohamed Hussein walikosa umakini katika kufunga. Kwa upande wa Ruvu Shooting, dakika ya 29, Full Maganga, alishindwa kuweka mpira wavuni akiwa hatua chache na lango la Simba, akipokea mpira wa kona uliopigwa na Shaaban Kisiga.

Ruvu Shooting walifanya shambulizi zuri dakika ya 31, lakini Jabir Azizi,  alishindwa kufunga  kutokana na kutokuwa makini huku akionyeshwa kadi ya njano dakika ya 38 kwa kumchezea rafu, Pastory Athanas.

Kichuya alipoteza nafasi nyingine dakika ya 40 baada ya kupiga shuti lililookolewa na mabeki wa Ruvu Shooting, kufuatia kazi nzuri aliyofanya Hussein.

Dakika mbili baadaye, Mzamiru Yassin  alishindwa kufunga akiwa katika mazingira mazuri lakini shuti lake lilitoka nje.

Ibrahimu alifunga bao dakika ya 45 baada ya kupiga shuti kwa mguu wa kushoto kufuatia krosi ya kiungo, Jonas Mkude, iliyotokana na mpira uliorushwa na Kichuya.

Kipindi cha pili Simba walifanya mabadiliko dakika ya 52 kwa kumtoa Mohamed Ibrahim na kuingia Juma Luizio na baadaye alitoka Kichuya na nafasi yake kuchukuliwa na Mwinyi Kazimoto dakika ya 68.

Ruvu Shooting walimtoa Jabir Azizi na kuingia Shaaban Masala dakika ya 75 na Simba  kumtoa Bukungu na kuingia Said Ndemla, lakini hawakuweza kubadilisha matokeo.

Simba: Daniel Agyei, Juvier Bukungu, Mohamed Hussen, Abdi Banda, Method Mwanjala, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Mzamiru Yassin, James Kotei, Pastory Athanas na Mohamed Ibrahim/ Juma Luizio.

Ruvu Shooting: Bidii Hussein, Abdul Mpambika, Yusuph Mguya, Renatus  Kaseke, Bakari Mtuwi, Jabir  Azizi, Shaaban Kisiga, Danas Hussen, Fully Maganga, Ismail Mohamed/ Chande Magoha na Ibrahim Mussa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -