Monday, August 10, 2020

SIMBA JEURI

Must Read

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi...

NA WINFRIDA MTOI

SHOO moja tu pekee ya kibabe aliyoonesha kiungo mshambuliaji wa Simba, Luis Miquissone, imetosha kuwapa jeuri Wekundu wa Msimbazi hao, wakidai inabidi viingilio vya mechi zao viongezwe ili kutende haki kiwango cha mkali wao huyo.

Luis kwa sasa ndiyo habari ya mjini ndani ya Simba, kiasi kwamba jina lake ndilo linalotajwa zaidi na wapenzi wa timu hiyo.

Cheche za mchezaji huyo alianza kuzionyesha rasmi katika mchezo wao wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar, uliopigwa Jumanne ya wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, ziliamsha hisia kali kwa Wanamsimbazi kiasi cha kujikuta wakikubali kuwa wamelamba dume.

Wadau wa timu hiyo, walikuwa wakisubiri kwa hamu kumuona nyota huyo akicheza kwa muda mrefu katika kikosi cha baada mechi chache alizocheza kuingia akitokea benchi.

Luis aliyesajiliwa na Simba katika kipindi cha dirisha dogo msimu huu, akitokea UD Songo ya Msumbiji alikokuwa akicheza kwa mkopo, akiwa ni mali ya Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini, alikuwa hajapata nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza tangu ametua Msimbazi.

Kitendo cha kushindwa kupata nafasi ya kuanza mapema, ni kama kiungo huyo anayemudu kucheza kama winga, alikuwa amehifadhi vitu vyake na kupania kuteka shoo siku atakayopewa mwanya wa kujinasafi kwa dakika zote.

Wekundu wa Msimbazi walikuwa na hamu kubwa ya kuona vitu adimu alivyowafanyia katika Ligi ya Mabingwa Afrika, akiwa ndiye aliyeing’oa Simba kwenye michuano hiyo kwa bao lake la mkwaju wa penalti uliotokana na rafu aliyochezewa baada ya kuwatesa vibaya viungo na mabeki wa timu hiyo.

Bila kujivunga, Luis ni kama alikuwa katika mioyo ya Wanasimba, kwani baada ya kusumbuliwa na watani wao, Yanga ambao walikuwa wakijinadi na Bernard Morrison kutokana na mtindo wake kutembea juu ya mpira ‘shibobo’, walitaka mtu wa kufanya vitu vya ajabu zaidi katika kikosi chao.

Katika mchezo huo wa Jumanne, Luis alionesha kiwango kikubwa cha kumiliki mpira, kupiga chenga na pasi zenye macho zinazokwenda mbele kutengeneza mashambulizi.

Kutokana na cheche hizo, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara, amelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Bodi ya Ligi kuongeza viingilio vya mechi zao kutokana na burudani inayotolewa na Luis pamoja na nyota wengine wa timu yao.

Katika ukurasa wake wa Instagram, Manara aliweka picha ya Luis na kuandika: “Ni dhambi kulipa pesa ile (sh 5,000) kumwangalia Luis akicheza, hata Azam TV ongezeni bei ya vifurushi vyenu. Jana (Jumanne) nilikuwa najiuliza, namuangalia Messi (Lionel) au? Sasa hivi kubaki nyumbani wakati Miquissone anacheza, ni kosa linaloweza kukuweka ndani.”

Mbali ya Luis, pia kiungo mwingine wa timu hiyo, Clatous Chama alionyesha kiwango cha hali ya juu kunogesha shoo ‘bab kubwa’ iliyotolewa na kikosi cha Simba katika mchezo huo ambao hata hivyo, walishinda kwa bao 1-0, mfungaji akiwa ni Meddie Kagere aliyecheka na nyavu kwa mkwaju wa penalti.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa timu hiyo kuwa atajituma na...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi katika klabu ya Simba kwa...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -