Sunday, January 17, 2021

SIMBA: JEURI YENU KWISHAAA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

*Watamba kurejea kileleni J’mosi, kuwasambaratisha Yanga Feb 25

NA ZAITUNI KIBWANA

SIMBA wameibuka kwa mara nyingine kuwakejeli mashabiki wa Yanga wakiwaambia kuwa jeuri yao ya kuendelea kutamba katika Ligi Kuu Tanzania Bara sasa imekwisha, lakini pia wakiwataka kujiandaa kupokea kipigo cha mbwa mwizi watakapokutana Februari 25, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Hata hivyo, Wekundu wa Msimbazi hao wameshindwa kuweka wazi ni vipi Yanga hawatakuwa na jeuri tena, wakati wachezaji walionao watani wao hao ni wale wale waliotwaa ubingwa msimu uliopita, kukiwa na mabadiliko katika benchi la ufundi baada ya kocha mkuu wao wa zamani, Hans van der Pluijm, kumpisha Mzambia, George Lwandamina.

Japo tangu awali Simba walikuwa wakionekana kuitambia Yanga, lakini tambo hizo zilizidi jana ambapo mashabiki wa timu hiyo kutoka maeneo mbalimbali waliliambia BINGWA kuwa wana uhakika mkubwa wa kutwaa ubingwa wa Bara kwani watani wao hao hawana jeuri tena ya kuwasumbua vichwa kama ilivyokuwa msimu uliopita.

Baada ya kikosi hicho cha Simba kushushwa kileleni na mahasimu wao Yanga, sasa wanatarajia kurejea kileleni Jumamosi hii watakapokutana na Tanzania Prisons kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mbwembwe zao za kurejea kileleni, pia wana uhakika wa kubakia kileleni mwa msimamo huo hadi kunyakua ubingwa kwa kuwa wapinzani wao hawatakuwa na makali yoyote kwao.

Simba walishushwa kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kuchapwa bao 1-0 dhidi ya Azam, wakitoka sare ya 0-0 dhidi ya Mtibwa Sugar na kuifanya Yanga kupanda kileleni wakiwa na pointi moja zaidi yao ambazo ni 49.

Akizungumzia maandalizi ya mchezo wao Meneja wa Simba, Musa Hassan ‘Mgosi’, alisema wana uhakika wa kushinda kila mechi bila kipingamizi chochote.

“Bila kushinda mechi zilizosalia ubingwa tutausikia kwenye bomba, hivyo tutaanza na Prisons wikiendi hii ili kuweza kuweka rekodi zetu sawa, kisha tutakuja kujipigia mahasimu wetu Yanga,” alisema.

Katika mchezo huo wa Jumamosi, Simba itawakosa wachezaji wao wawili, Abdi Banda, ambaye ni majeruhi akisumbuliwa na kifundo cha mguu na Jamal Mnyate anayesumbuliwa na maumivu ya goti.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -