Sunday, October 25, 2020

SIMBA JITOKEZENI MFANYE UCHAGUZI WA HAKI

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA ZAITUNI KIBWANA


MCHAKATO wa uchaguzi wa viongozi wa klabu ya Simba umeanza rasmi wiki hii ambapo wadau mbalimbali wameonyesha nia ya kuchukua fomu za kuwania uongozi.

Uchaguzi huu umepangwa kufanyika Novemba 3 na utahusisha wajumbe sita ambao wataingia moja kwa moja kwenye bodi ya wakurugenzi watakaoungana na wale wa Mohammed Dewji ambaye naye atateua wajumbe wanane.

Simba ambayo ilifanya mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji kutoka wanachama hadi wa uuzaji hisa ambapo sasa mfanyabiashara, Mohammed Dewji ‘Mo’ ndiye mmiliki baada ya baraka zote za kumiliki hisa 49% na 51% zikibaki kwa wanachama.

Kuelekea kwenye uchaguzi huo sifa kuu za kugombea nafasi ya mwenyekiti ni  lazima uwe na elimu ngazi ya shahada na wajumbe wanne wanatakiwa kuwa na elimu ya kidato cha nne.

Licha ya zoezi hilo kuanza mpaka jana hakuna hata mwanachama mmoja aliyejitokeza huku fomu ya nafasi ya Mwenyekiti zikitolewa kwa Sh 500,000 wakati nafasi za wajumbe ambao wanaingia moja kwa moja kwenye bodi ya wakurugenzi ni Sh 300,000.

Zoezi hilo litakamilika Septemba 11, kabla ya wagombea kurudisha fomu hizo kuanzia Septemba 11-15.

Ikumbukwe hii ni haki ya kikatiba ya Simba kwa wanachama wenye sifa kujitokeza kuwania uongozi kwenye uchaguzi huo ambao viongozi ambao  watapatikana watakaa madarakani kwa miaka minne.

Kama zilivyo chaguzi nyingine za kawaida, mambo mengi yanatokea katika kipindi cha mchakato wa uchaguzi mpaka kufikia siku yenyewe ya uchaguzi kwa kuwa kila mmoja anatafuta nafasi ya kuingia ndani ya uongozi wa klabu hiyo.

Matukio ambayo mara kwa mara yamekuwa yakilalamikiwa wakati wa mchakato na mpaka kufikia siku ya uchaguzi ni pamoja na rushwa, kampeni chafu pamoja na hila mbalimbali kutoka kwa wagombea.

Tunawakumbusha Kamati ya uchaguzi ya Simba, wagombea pamoja na wajumbe wa Mkutano Mkuu ambao watapiga kura kuchagua viongozi, tunataka kuona uchaguzi wa huru na haki.

Tunaamini viongozi watakaochaguliwa watakuwa wamepata kura nyingi miongoni mwa wagombea wote katika uchaguzi.

Hivyo ni vizuri atakayeshinda apewe nafasi yake ya ushindi na pasiwe na figisu figisu kwa kuwa Watanzania na wadau wa soka wanataka kiongozi atakayekuwa na mapenzi mema na soka letu.

Tunaomba kamati ya uchaguzi kuhakikisha kila kitu kinafanyika katika maadili yanayokubalika na kanuni za uchaguzi huo.

Kwa upande wao wagombea, hakuna haja ya kuwapo na kampeni za matusi kwa kuwa hiyo haitamjenga mgombea na haitashawishi wajumbe kuwapigia kura za kuwaweka madarakani.

Tunataka mgombea aeleze kinagaubaga ahadi zake badala ya kutoa kejeli na vijembe ambavyo havitasaidia chochote.

Hatutarajii kusikia wagombea wakishambuliana na kuchafuana wao kwa wao kwa masuala binafsi ambayo hayana msingi kwa wanachama wanaomtaka mtu atakayesaidia maendeleo ya soka letu.

Kwa upande wa wajumbe wa mkutano mkuu ambao ndio wanabeba dhamana ya wadau wote wa soka, wanapaswa kuchagua viongozi sahihi watakaotupa mafanikio.

Kwa wagombea wanapaswa kufahamu sera zao na mipango madhubuti ambayo waliinadi ndiyo itawawezesha kuingia madarakani na wala si kwa kutaka kupitia njia za panya kama ilivyokuwa ikidaiwa katika chaguzi zilizopita.

Tunahitaji kuona soka letu linapiga hatua kuliko lilipo kwa sasa, kwani furaha ya Watanzania si kuona mpira unachezwa hapa nchini bali unapata maendeleo hadi ngazi za kimataifa.

Ili hilo lifanikiwe wajumbe ndio wamebeba dhamana ya wadau wote wa soka kuchagua viongozi, hivyo wanapaswa kuwa makini  kuchagua watu sahihi ambao watatuletea maendeleo na mafanikio katika tasnia hiyo.

Tunawatakia kila la heri wale wote watakaochukua fomu za kuwania uchaguzi, tunawatakia mchakato mwema wa uchaguzi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -