Sunday, November 29, 2020

SIMBA, KAGERA HATUMWI MTOTO DUKANI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

SAADA SALIM NA KYALAA SEHEYE

GUMZO kubwa kanda ya ziwa kwa sasa katika Ligi Kuu Tanzania Bara ni mechi ya Simba dhidi ya Kagera Sugar, mchezo utakaopigwa katika Uwanja wa Kaitaba, mkoani Kagera.

Katika mchezo huo, Simba inahitaji pointi tatu muhimu ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kuendelea kabaki kileleni ambapo tayari amejikusanyia pointi 55, huku Yanga ikiwa nafasi ya pili kwa pointi 53 katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Ni mechi muhimu sana kwa upande wa Simba kuhakikisha safu yake ya ushambuliaji inayoongozwa na Mrundi Laudit Mavugo anakuwa makini kuichambua safu ya ulinzi ya Kagera kuhakikisha wanaibuka na ushindi.

Simba inashuka dimbani ikiwa na jeshi kamili kuhakikisha wanapata pointi muhimu ili kuendelea kuwaacha wapinzani wao, Yanga katika nafasi ya pili, ambao nao wanatetea taji la ubingwa.

Kwa Simba inahitaji kuweka mambo sawa, hakuna timu hata moja kati ya Yanga yenye nafasi kubwa zaidi ya kubeba ubingwa zaidi ya mwenzake kulingana na hali halisi ilivyo.

Pointi mbili, hata ingekuwa mechi mbili zimebaki, si jambo la upande wowote kuona uko salama. Katika mechi hii dhidi ya Kagera, Simba inatakiwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo huo ambao utawaweka salama.

Hapa Simba akifungwa, Yanga akishinda mambo yanabadilika kabisa, lakini inawezekana hiyo faida ya Simba ikaanza kuonekana kama Yanga hawatashinda dhidi ya Azam.

Yanga wakiona Simba inacheza na Kagera, wanaweza kwenda kutoa sapoti kwa timu hiyo inayonolewa na Mecky Mexime ipambane ili kuhakikisha inaizuia Simba.

Katika misimu mitatu iliyopita, wamekutana mara saba, huku Simba ikiwa imeshinda mara nne, sare mara moja na kufungwa mechi mmoja katika uwanja huo wa Kaitaba.

Simba, ambayo inanolewa na Mcameroon Joseph Omog, kocha huyo atahakikisha anakipanga kikosi chake vyema kwa ajili ya kupata ushindi ambapo safu yake ya ushambuliaji ikiongozwa na Mavugo, Ibrahim Ajib na Shiza Kichuya, itahakikisha haitoki kapa.

Wakati huohuo, Kagera Sugar inatarajiwa kuongozwa na kipa Juma Kaseja, atakayehakikisha anawadhibiti vilivyo washambuliaji wa Simba kuleta madhara katika timu yao.

Wakizungumzia mchezo huo kwa nyakati tofauti, Mavugo alisema wanahitaji ushindi, kwani lengo lao ni kuhakikisha wanafikia mikakati yao ya kutwaa ubingwa.

Alisema ana imani kubwa na wenzake kufanya vizuri, kwani kila mmoja amepewa jukumu lake, hivyo wanaingia uwanjani kupambana kuhakikisha wanapata pointi muhimu.

“Kikubwa ni pointi tatu, tumepokea maelekezo ya kocha na kuyafanyia kazi, mashabiki waendelee kutusapoti, kwani tunaendelea kuwapa raha,” alisema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -