Thursday, November 26, 2020

Simba: Kazi iliisha Mwanza

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ASHA KIGUNDULA 

SIMBA wamesema pointi tatu ni lazima kesho dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga, kwani mchezo ulishamalizika toka Jumanne wiki hii kwenye Uwanja wa Gwambina Complex, Mwanza.

Yanga ilicheza na Gwambina Jumanne kwenye Uwanja wa Gwambina Complex, ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ulioshia kwa timu hizo kutoka suluhu.

Wakati Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze akisema matokeo ya Jumanne yalikuwa ni ya kimchezo tu, kumbe kwa upande wa Simba yalikuwa na maana kubwa kwao kuelekea pambano la watani wa jadi kesho kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.

Simba wamesema kuwa japo awali walikuwa na matumaini ya kuichapa Yanga kesho, lakini kitendo cha watani wao hao wa jadi kuambulia pointi moja Jumanne Gwambina Complex, kimezidi kuwapa nguvu ya kushinda kesho.

Akizungumza na BINGWA jana, Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, alisema kuwa vijana wake watashuka dimbani kesho kuivaa Yanga, wakifahamu ushindi utawawezesha kupunguza pengo la pointi baina yao na watani wao hao.

Alisema kuwa awali walikuwa na mnlima mrefu wa kupanda kuipita Yangam, walipokuwa wameachwa kwa pointi sita, lakini baada ya suluhu ya watani wao hao Jumanne, jijini Mwanza, sasa kazi iliyobaki mbele yao ni rahisi mno.

Alisema kuwa watambua wakiichapa Yanga, pengo la pointi baina yao litakuwa ni pointi moja tu, hivyo ahwawezi kukubali kuipoteza kirahisi fursa hiyo.

Endapo Wekundu wa Msimbazi hao, watafanikiwa kuibuka na ushindi kesho, watakuwa wanadaiwa pointi moja mabayo ni rahisi kuipata katika mechi zijazo.

Mzuka wa Simba, umechangiwa pia na ushindi waliopata dhidi ya Kagera Sugar kwa kuifunga mabao 2-0 juzi na kuchukua alama tatu muhimu.

Wanamsimbazi hao wanaamini ubora wa nyota wao na morali iliyopo, ni wazi uwezo wa kushinda mtanange huo wa kesho wanao, ukizingatia mechi ya mwisho walipokutana waliibuka kidedea kwa kuichapa Yanga mabao 4-1.

Akizungumza mara ya mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Sven alisema kuwa wanatambua mchezo dhidi ya Yanga ni mgumu, lakini watapambana wapate ushindi.  “Jumamosi tunahitaji ushindi tuweze kuwa na tofauti ndogo ya pointi dhidi ya Yanga, najua utakuwa mchezo wa ushindani, lakini ninakiamini kikosi changu, kitapambana kipate pointi tatu,” alisema Sven. Alisema licha ya kuwa na wachezaji wake kadhaa ni majeruhi, waliopo watapambana kuibeba timu yao iweze kujiweka pazuri katika harakati zao za kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa msimu wa nne mfululizo.    Licha ya kuwa na majeruhi wa muda mrefu kama vile Gerson Fraga na Meddie Kagere, Simba ina nyota wao wengine walioumia juzi ambao ni Clatous Chama, Shomari Kapombe na Ibrahim Ame ambao wapo chini ya uangalizi wa madaktari.        Mchezo wa kesho wa raundi ya 10 baina ya watani hao wa jadi, utaanza saa 11:00 jioni.    Katika msimamo wa ligi hiyo, Yanga wanaongoza wakiwa na pointi 23 baada ya kucheza mechi tisa sawa na Simba waliopo nyuma yao na pointi zao 19. Azam wenye pointi 22, wakiwa wamecheza mechi tisa, wapo nafasi ya pili.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -