Saturday, November 28, 2020

SIMBA KICHEKO KILA KONA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAITUNI KIBWANA

JAPO bado kuna safari ndefu kuelekea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, mashabiki wa Simba kila kona ya nchi, wameonekana kuwa na uhakika mkubwa wa kubeba taji, lakini jeuri yao hiyo ikionekana kusababishwa na ubora wa kikosi chao kilichosheheni wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu.

Na zaidi, jeuri hiyo imetokana na ushindi wa mabao 2-1 walioupata mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga.

Kikubwa zaidi, ushindi huo mnono waliupata wakati timu yao ikiwa pungufu ya mchezaji mmoja, baada ya beki wao wa kulia, Janvier Bokungu, kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi mshambuliaji wa Yanga, Obrey Chirwa.

Na sasa wakati Wekundu wa Msimbazi hao wakitarajiwa kushuka dimbani leo kumenyana na Mbeya City ya Mbeya kwenye Uwanja wa Taifa, mashabiki wake wana uhakika mkubwa wa kutoka uwanjani na pointi zote tatu kabla ya kuendelea kufanya hivyo kwenye mechi zao zinazofuata.

Katika mitandao ya kijamii, vijiwe na vyombo vya usafiri, mashabiki wa Simba wanaamini pengo la pointi mbili baina yao na Yanga wanaoshika nafasi ya pili, nyuma yao, litaendelea vivyo hivyo hadi ligi hiyo itakapofikia ukingoni na hatimaye Wekundu wa Msimbazi hao kutangazwa mabingwa wapya wa Bara.

Katika hilo, Simba imeweka mikakati ya hali ya juu kuhakikisha hawafanyi kosa katika mechi zao zote saba zilizobaki za ligi, ili kuepuka kushuka kileleni na kutoa mwanya kwa Yanga kutetea ubingwa wao.

Kocha wa Simba, Joseph Omog, ameonekana kuwa makini na hali ilivyo sasa kwenye mbio za ubingwa, hivyo kuweka mikakati ya kutwaa pointi tisa ndani ya Kanda ya Ziwa, ili kuweka mipango yao sawa.

“Ubingwa upo Kanda ya Ziwa, ili kutimiza ndoto hizo, natakiwa kupata pointi tisa huko, ambapo kama nikishinda basi nitakuwa salama zaidi na kushusha presha ya mbio za ubingwa,” alisema Omog.

Mechi za Simba za Kanda ya Ziwa ni dhidi ya Toto Africans, Mbao FC na Kagera Sugar, ambazo zote ni ngumu zikihitaji nguvu na mikakati ya ziada.

Kati ya hizo, mechi dhidi ya Toto ndiyo inayotajwa kuwa ngumu zaidi, kutokana na historia, kwani mara nyingi Simba imekuwa ikiambulia kipigo inapokutana na vijana hao wa Rock City kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.

Ukiachana na mechi hizo, pia kuna vipute dhidi ya African Lyon, Stand United na Mwadui FC, ambavyo navyo si vya kubeza kwa Wekundu wa Msimbazi hao.

Juu ya mchezo wao wa leo, Simba wanatarajiwa kutumia mbinu na mikakati ile ile waliyoitumia kuiangamiza Yanga Februari 25, mwaka huu, kuhakikisha wanatoka uwanjani na ushindi dhidi ya ‘wabishi’ hao wa Mbeya ambao si wa kubeza.

Tayari Mbeya City kupitia kwa kocha wao, Kinnah Phiri, imetamba kuishangaza Simba leo ikitamba Wekundu wa Msimbazi hao si lolote kwao.

Ikumbukwe kuwa, Simba imejikuta katika ukame wa mataji baada ya kumaliza misimu minne bila kutwaa kombe lolote, ikiishia kuzikodolea macho Yanga na Azam zikijinafasi katika nafasi mbili za juu.

Simba ndiyo inayoongoza katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 54, kutokana na michezo 23 iliyocheza, sawa na Yanga ambayo yenyewe ina pointi 52.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -