Friday, November 27, 2020

SIMBA KIDEDEA SAKATA LA KESSY

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAITUNI KIBWANA

WEKUNDU wa Msimbazi, Simba, wameibuka kidedea kwenye sakata la beki wao, Hassan Ramadhani ‘Kessy’, baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwataka Yanga kulipa Sh milioni 50 kama fidia.

Uamuzi huo umetolewa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF chini ya Mwenyekiti wake, Richard Sinamtwa, baada ya kusikiliza pande zote mbili.

Akithibitisha kutakiwa kutolewa fedha hizo, Msemaji wa TFF, Alfred Lucas, alisema kuwa Yanga imetozwa faini ya Sh milioni tatu kwa mujibu wa kanuni na fidia kwa Simba ya Sh milioni 50.

Alisema mbali na faini hiyo, Yanga wamekutwa na kosa la kupeleka jina la Kessy CAF, huku akiwa ana mkataba na Simba uliokuwa unaishia Juni 15, mwaka huu.

“Kitendo cha Yanga kupeleka jina la Kessy CAF akiwa ndani ya mkataba na Simba, ni kosa kubwa kwa mujibu wa kanuni za ligi kifungu 69 (5) ambalo linapaswa kupewa adhabu itakayopelekea wanachama wote kuheshimu nafasi ya TFF kwenye suala la usajili na si kuanza kwenda CAF au kwingineko ili kulinda heshima ya soka la Tanzania.

Alisema mbali na faini hizo, pia Ofisa wa TFF ambaye hajatajwa jina aliyehusika kushirikiana na uongozi wa Yanga kufanikisha usajili huo wa Kessy, atachukuliwa hatua za kinidhamu na Katibu Mkuu, Selestian Mwesigwa.

“Ofisa huyo kwa kushirikiana na Yanga au kwa kutochukua hatua stahiki kwa wakati, apelekwe kwenye mamlaka yake ya nidhamu, yaani awajibishwe na Katibu Mkuu wa TFF,” alisema.

Kufuatia hukumu hiyo, BINGWA lilimtafuta Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hans Pope, kuzungumzia sakata hilo kama wamekubaliana na fedha hizo, ikiwa ni baada ya awali kutaka Dola za Marekani 600,000 (zaidi ya Sh bilioni 1.2) ambapo alisema: “Sawa tu tulijua hivyo maana tungesema milioni 50 tungepata milioni 10 tu na yeye alikuwa amebakisha mwezi mmoja tu huku tukiwa tumemsajili kwa Sh milioni 30 miaka miwili. Si haba,” alisema Hanspope.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -