Saturday, October 31, 2020

SIMBA KUENDELEZA WEMBE ULE ULE

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

SALMA MPELI NA ZAINAB IDDY

SIMBA wanajua kuwa wamewapita Yanga kwa pointi mbili tu na wakizubaa wanashushwa kileleni na kwa kutambua hilo wamewaambia maafande wa JKT Ruvu, wakirogwa wakaingiza timu uwanjani watawaangamiza kabisa.

Wekundu hao wa Msimbazi watakutana na JKT Ruvu mwishoni mwa wiki hii, Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, mchezo unaotarajiwa kuwa mkali kila timu ikihitaji kuondoka na pointi zote tatu.

Kikosi hicho ambacho kinanolewa na Joseph Omog, ndicho ambacho kipo kileleni mwa msimamo kikiwa na pointi 38 huku watani zao wa jadi, Yanga wakiwafuatia kwa ukaribu na pointi 36.

Katika mchezo wa mzunguko wa kwanza timu hizo zilipokutana zilijikuta zikitoshana nguvu na kutoka suluhu ya 0-0 kitu ambacho Simba hawataki kijirudie tena mzunguko huu wa lala salama.

Akizungumza na BINGWA jana jijini Dar es Salaam, kocha msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja, alisema hawataki kurudia makosa yaliyojitokeza kwenye mzunguko wa kwanza hivyo wamejipanga kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo.

“Tulipokutana mzunguko wa kwanza tulitoka sare tasa na sasa tunakwenda kukutana tena nao mzunguko huu wa pili, imani yangu ni kwamba tutafanya vizuri na kuondoka na pointi zote tatu ili tuzidi kukaa juu,” alisema.

Wekundu hao wa Msimbazi wanayo misimu minne mfululizo bila kunusa harufu ya ubingwa na kushindwa kabisa kushiriki michuano ya kimataifa ikiziangalia Yanga na Azam zikibadilishana nafasi za juu na sasa hawataki tena hayo yajitokeze.

Tangu msimu huu uanze wekundu hao wa Msimbazi wanaonekana wazi kupania kutwaa ubingwa huo kutokana na kandanda la kuvutia wanalolionyesha na pia matokeo mazuri wanayoyapata kitu ambacho kinawapa moyo mashabiki.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -