Thursday, December 3, 2020

SIMBA KUSAKA POINTI 15 ZA JASHO NA DAMU

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA ZAITUNI KIBWANA

SIMBA sasa inalazimika kuzisaka pointi zote 15 zilizosalia kwa jasho na damu ili kujihakikishia nafasi ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara msimu huu.

Wakati Simba ikihitaji kupata pointi hizo kutoka kwenye mechi tano zilizosalia, inaomba Yanga angalau ipoteze mchezo mmoja ndipo hesabu zao ziende sawa katika kutwaa taji hilo walilolikosa kwa miaka minne.

Simba ilipoteza mchezo wake muhimu dhidi ya Kagera Sugar mwishoni mwa wiki mjini Bukoba na kutoa nafasi ya mahasimu wao wa Jadi Yanga kuendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi, wakiwa na pointi moja mbele huku timu zote zikiwa na mechi sawa.

Kwa hali hiyo kama Simba itashinda zote na Yanga kushinda zote, bado Yanga itakuwa Bingwa kwa sababu wana pointi moja mbele ya Simba, hivyo Simba wameamua ni kufa na pointi zote 15 bila kujali Yanga wanapata matokeo gani kwenye mechi zao.

Mechi hizo ambazo Simba wanazipigia hesabu na dua ni dhidi ya Toto Africans, Mbao FC zitakazofanyika Kanda ya Ziwa na African Lyon, Stand United na Mwadui FC.

Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja wa Simba, Mussa Hassan ‘Mgosi’, alisema mechi tano zilizosalia ndizo zitakazoamua kama kikosi hicho kitatwaa ubingwa au la, hivyo watatumia nguvu ile ile waliyoitumia kwenye mechi zilizopita ili kukusanya pointi tatu muhimu.

Alisema hajakata tamaa ya ubingwa na kilichopo mbele yao ni kuhakikisha wanashinda mechi zote tano kisha wataangalia wamefanikiwa kupata nini mwishoni mwa ligi.

“Kuna watu wanasema Yanga akiwa juu hakuna wa kumshusha, hivi ni nani alijua kama tutafungwa na Kagera, mpira una matokeo matatu na lolote linaweza kutokea wala hatujakata tamaa,” alisema.

Akizungumzia maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Mbao FC, Mgosi alisema kikosi hicho kinaendelea na mazoezi ili kuhakikisha wanaibuka na pointi tatu katika mchezo huo.

“Tunafanya mazoezi ambapo hata majeruhi Method Mwanjali ameanza mazoezi, hivyo kwetu sisi kila mechi ni fainali tunataka pointi tatu,” alisema.

Simba ambao wamekusanya pointi 55 wakishika nafasi ya pili, huku wapinzani wao Yanga wakiongoza msimamo huo wa Ligi kwa kukusanya pointi 56 baada ya kushuka dimbani mara 25.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -