Wednesday, October 28, 2020

SIMBA KUSHUSHA MUZIKI KAMA WOTE

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

SAADA SALIM NA DEBORA MBWILO, TUDARCO


MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba, wameonyesha kwamba hawataki masihara kwa kuhakikisha hawaporwi taji hilo la Ligi Kuu na leo watautumia mchezo wao wa kirafiki dhidi ya AFC Leopards ya Kenya kuzidi kujiweka sawa.

Simba watacheza mchezo huo wakizidi kunoa wachezaji wao kwa mechi zijazo za Ligi Kuu, ukiwamo mchezo wao dhidi ya Yanga, utakaochezwa Septemba 30, mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini jana, mlinda mlango Simba, Deogratius Munishi `Dida`, alisema mchezo huo kwao ni wa muhimu katika mwendelezo wa maandalizi ya Ligi Kuu.

“Tumejiandaa vizuri na tupo tayari kwa mchezo wetu huo wa kirafiki, nina imani utatoa taswira nzuri kwa benchi la ufundi kuona mapungufu na kufanyia kazi kabla ya kwenda katika mechi za Ligi Kuu,” alisema Dida.

Pia mlinda mlango huyo alikilaani kitendo cha baadhi ya mashabiki wa Simba kudai wataishangilia Uganda katika mchezo wa kufuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) dhidi ya Taifa Stars.

Dida amewaonya mashabiki hao akisema kitendo hicho si cha kiungwana na wala hakifurahishi kutokana na wao wapo Tanzania.

“Wakiamua kuwashangilia Uganda, basi watambue wanatuvunja moyo, wanatakiwa kutusapoti kwa kuonyesha ushirikiano, kwani watambue wachezaji wanaocheza Stars wanatumikia taifa na si klabu,” alisema.

Hatua hiyo ya baadhi ya mashabiki wa Simba kutaka kuiunga mkono Uganda inatokana na kitendo cha kocha wa Stars, Emmanuel Amunike, kuwatema wachezaji sita wa Wekundu hao wa Msimbazi kwa kitendo cha kuchelewa kuingia kambini.

Hivyo Dida aliwataka mashabiki kuonyesha uzalendo katika suala hilo, kwani wakichukua maamuzi ya kushangilia wapinzani wao wanavunjika moyo.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wake, Haji Manara, Watanzania wote wanapaswa kuwa kitu kimoja kwa kuonesha utaifa na uzalendo kwa Stars, ambayo itakuwa inaiwakilisha nchi.
Kwa upande wa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Simba, Haji Manara, alisema kikosi hicho kinaendelea vizuri kwa ajili ya mchezo huo.

“Mchezo huo wa kirafiki umetakiwa na kocha, hivyo kwetu ni muhimu sana, kabla ya kwenda kucheza mechi dhidi ya Ndanda na nyingine kwa kuhakikisha kikosi chake kinakuwa vizuri kwa ajili ya kusaka pointi muhimu,” alisema Manara.

Pia Manara aligusia sakata hilo la baadhi ya mashabiki wa Simba kutaka kuishangilia Uganda, akisema atawashangaa kama watafanya hivyo, kwa kuwa sababu yao haina maana.

Manara pia amefunguka kwa kusema sababu ya uwepo wa wachezaji wao, Jjuuko Murshid na Emmanuel Okwi kwenye kikosi cha Uganda, isiwe sababu ya kuikacha Stars na badala yake akiwataka waweke utaifa mbele.
Kwa upande wa Nahodha wa AFC Leopards, Aziz Okaka, alisema wanatambua Simba ni timu kubwa na ina wachezaji wazuri, lakini hata yao ni kubwa nchini Kenya.

“Tumekuja kucheza mechi hii ya kirafiki, tunatambua Simba ni timu kubwa na sisi pia ni timu kubwa Kenya, lakini tunahitaji kufuta uteja wetu kwao kwa kila tunapocheza wanatufunga,” alisema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -