Friday, December 4, 2020

SIMBA, LYON MCHEZO WA KISASI

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA EZEKIEL TENDWA,

TIMU ya Simba na African Lyon leo zitashuka katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kumenyana katika mchezo wa raundi ya sita wa Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup).

Katika raundi hiyo ya sita, ni mchezo mmoja tu utachezwa leo, huku mingine ikitarajiwa kuchezwa mwishoni mwa wiki ijayo, huku mchezo huo ukiwa muhimu kutokana na kuwa bingwa atapata nafasi ya kuwakilisha nchi katika Kombe la Shirikisho barani Afrika, ambayo bingwa wa ni TP Mazembe ya Congo.

Msimu uliopita, Yanga ndio waliofanikiwa kutwaa ubingwa huo kwa kuwafunga Azam FC, ambao ndio waliachiwa nafasi ya kushiriki michuano hiyo kutokana na kuibuka mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kupata nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu na wa kisasi baada ya Simba kufungwa na Lyon kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, huku kikosi hicho cha Lyon kikitaka nafasi ya kuwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa.

Akizungumzia mchezo huo, kocha wa Simba, Joseph Omog, alisema wanataka ushindi ingawa anajua watakutana na upinzani mkubwa kutokana na ubora walionao African Lyon.

Katika mchezo wa leo, Simba itaendelea kuwategemea washambuliaji wake tegemeo, Laudit Mavugo, Ibrahim Ajib pamoja na Juma Luizio ambao kwa sasa wameonekana kuwa tishio.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -