Sunday, October 25, 2020

SIMBA MKIJICHANGANYA KWA MAVUGO, YANGA WATAWALIZA

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA SAADA SALIM,

PAMOJA na ukongwe wa klabu ya Simba, lakini imeshindwa kuwa wavumilivu kabisa hasa kwa wachezaji wao.

Mara inapotokea wachezaji wao hawafanyi vizuri wamekuwa wakiwazodoa, badala ya kukaa na kutafakari tatizo ama changamoto zinazowafanya nyota wao kushindwa kufanya vizuri.

Kwa muda mrefu sasa mashabiki wa klabu ya Simba wamekuwa wakimtupia lawama mshambuliaji wao, Laudit Mavugo.

Lawama hizo zinakuja kutokana na Simba kutegemea kupata mabao kutoka kwa viungo wao kuliko mshambuliaji huyo wa Burundi.

Kwa kitendo hicho cha mashabiki kumwona Mavugo hafai, kinaweza kusababisha uongozi kukurupuka na kumwacha mshambuliaji huyo.

Lakini kama Simba haijajifunza kwa akina Elias Maguli na Amissi Tambwe, ambao waliwaacha kwasababu ambazo hazieleweki, basi wakijichanganya kumwacha na Yanga kumnasa watajuta kumfahamu.

Maguli alikuwapo Simba kabla ya kutua Stand United alikofanya vizuri na kutimkia Oman. Kwa upande wa Tambwe, bila shaka hakuna shabiki wa Simba asiyejua kilichowapata kwa mchezaji huyo ambaye tangu aondoke ameshawafunga mara tatu kwenye mechi za mahasimu hao.

Ikiwa Simba watarudia kosa hilo kwa Mavugo, basi majanga yatakayowapata yatakuwa makubwa kuliko yanayoendelea kusababishwa na Tambwe.

Mavugo alitua Simba baada ya kiwango kizuri alichokionesha Burundi, lakini baada ya mzunguko wa kwanza na huu wa pili kuanza kiwango chake kimefifia na kuwakatisha tamaa mashabiki wanaoanza kulia kwamba anatakiwa kuachwa katika kikosi cha timu hiyo.

Mavugo ni mchezaji mzuri sana tofauti na inavyodhaniwa na mashabiki wa Simba, kwani ana kila sifa anazopaswa kuwa nazo mchezaji.

Lakini ni kwanini Mavugo anashindwa kufanya vizuri? Kuna mambo kadhaa ambayo yanamfanya mshambuliaji huyo aonekane kuwa butu.

 Saikolojia

Mpaka sasa saikolojia ya Mavugo haiwezi kuwa sawa kwani ukilinganisha na Mavugo yule aliyeichezea Simba kwa mara ya kwanza katika mechi ya kirafiki dhidi ya FC Leopards ya Kenya, ni tofauti kabisa na huyu wa sasa.

Katika mchezo huo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kwenye sherehe za ‘Simba Day’, Mavugo alitokea benchi na kufunga bao moja na kutoa ‘asisti’ moja na kusababisha moja.

Lakini kutokana na kutopewa muda wa kutosha wa kucheza tangu amekuja, mchezaji huyo ameshindwa kufanya vizuri.

Benchi la ufundi la Simba lilipaswa kumpa muda wa kutosha mchezaji huyo ili aweze kuzoea ligi pamoja na kuzoeana na wenzake.

Mchezaji huyo amekuwa akianza mara chache na kutolewa, ama kuingia dakika chache kabla ya mpira kumalizika na kama amewahi kucheza dakika zote 90, basi huenda ikawa ni mechi moja pekee.

Hilo ni tofauti kabisa kwa upande wa Yanga, ambao wamekuwa wakiwapa wachezaji wao nafasi ya kutosha na matokeo yake wanavuna matunda.

Mmoja wa wachezaji wa Yanga ambao mwanzoni walionekana kama magarasa ni Donald Ngoma, ambaye sasa amekuwa staa wa kikosi hicho, huku Obrey Chirwa akianza kuwateka mashabiki wa klabu yake taratibu.

Kutojiamini

Kutokana na kutopewa nafasi ya kutosha uwanjani, huku mashabiki wengine wakizodoa uchezaji wake, imemsababishia kupoteza kujiamini.

Hivyo kelele hizo zimefanikiwa kumvuruga mchezaji huyo na sasa kutoonekana na msaada mkubwa katika kikosi cha timu hiyo.

Jambo pekee kwa mchezaji huyo wa zamani wa Vital’O ya Burundi analotakiwa kufanyiwa ni kupewa muda wa kutosha uwanjani, ili aweze kuonyesha ule uwezo ambao uliwafanya mashabiki wengine wa Simba waanze kumfananisha na mchezaji wao wa zamani, Emmanuel Okwi.

Pamoja na kocha wa Simba, Joseph Omog, kuelewa kwamba Mavugo ana uwezo mkubwa na huwasumbua mabeki, lakini haieleweki ni kwanini anashindwa kumpa nafasi.

Mfumo

Suala lingine ambalo linamfanya Mavugo ashindwe kuonyesha kiwango chake ni mfumo unaotumiwa na Simba.

Uchezaji wa Simba unaonekana kujaza sana viungo katika eneo la kati, huku wakiwaacha washambuliaji wao mbele bila ya msaada.

Ingawa Mavugo ni mchezaji mwenye kasi, nguvu na ana uwezo wa kupiga chenga, lakini hawezi kupambana peke yake na mabeki zaidi ya watatu.

Simba wamekuwa wakibakiza mshambuliaji mmoja mbele ambaye hukosa msaada pindi mpira unapopigwa mbele kwani hujikuta amezungukwa na mabeki, hakuna mtu wa kuiba mipira baada ya mshambuliaji kugongana na mabeki.

Mfumo huo wa Simba si tatizo kwa Mavugo pekee, bali ni sumu hata kwa klabu hiyo kushindwa kupata matokeo mazuri na ikiwa wameshinda basi ni bao moja ama mawili.

Simba inaonekana kama inacheza mfumo wa 4:4:2, lakini kwa jinsi wanavyojipanga na namba 10 wao kushuka kucheza sana katikati na viungo wengine, huku mawinga kuishia kwenye mstari wa kati inawafanya mfumo wao uonekane kama wanacheza 4:5:1.

Hivyo ni ngumu kuweza kufanikiwa kwa mfumo huo, pia ni ngumu sana kuona makali ya Mavugo.

Lakini kama Simba wakijichanganya na kumdharau Mavugo akatua Yanga, basi ujue itakuwa kiama chao.

Kutokana na mfumo wa Yanga na jinsi wanavyocheza kwa kushambulia, huku wakiwa na tabia ya kuwaamini wachezaji na kuwapa nafasi basi Simba wakijichanganya na kumwachia Mavugo watatia akili.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -