Monday, August 10, 2020

Simba, Namungo zatambiana

Must Read

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi...

NA ASHA KIGUNDULA, SUMBAWANGA

KOCHA Msaidizi wa Simba, Seleman Matola, amesema wapo tayari kwa ajili ya mchezo wao fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) dhidi ya Namungo FC kesho kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, mjini hapa.

Akizungumza na gazeti hili jana, Matola alisema wanahitaji kumaliza fainali hiyo ‘mapema’ ili kukamilisha malengo yao ya kutwaa taji la tatu msimu huu na la pili chini ya Mbelgiji, Sven Vandenbroeck.

Matola alisema wachezaji na benchi la ufundi wako tayari kwa mchezo huo ambao hautakuwa na presha kubwa kwa sababu tayari timu zote mbili zimeshakata tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao.

Kocha huyo alisema wamejiandaa kupambana ili kuweka heshima ya klabu yao, kabla ya kuanza maandalizi ya msimu mpya.

“Tulifika Sumbawanga tangu jana (juzi) jioni na leo (jana) jioni tutafanya mazoezi mwepesi ya mwisho. Kila mchezaji anajua tunahitaji kurudi na ushindi, ingawa tumewaambia Namungo ni timu nzuri na yenye wachezaji wenye kasi, hivyo lazima tuthibitishe ubora wetu wa msimu mzima,” alisema Matola.

Nahodha wa Simba, John Bocco, alisema wamejiandaa kucheza kwa kiwango cha juu ili kuhakikisha wanapata ushindi na kuongeza mataji msimu huu.

Bocco alisema watacheza kwa umakini kwani wanawaheshimu Namungo kutokana na ushindani waliouonyesha katika mechi zote mbili walizokutana msimu huu licha ya kuwa wageni Ligi Kuu Bara.

Kwa upande wake, Kocha Mkuu wa Namungo, Thierry Hitimana, alisema kikosi chake kimejiandaa kukutana na ushindani kwa sababu watacheza dhidi ya timu bora na yenye wachezaji wenye uzoefu wa mechi za michuano mbalimbali.

Hitimana alisema wataingia uwanjani kuwavaa Simba kwa tahadhari na wamejipanga kuwazuia wachezaji wao wanaoanzisha mashambulizi.

“Ni mechi kubwa, lakini fainali huwa haina mwenyewe, ukitumia vema nafasi na ujaribu kupunguza makosa, una nafasi nzuri ya kupata ushindi, tunamuomba pia Mungu awe upande wetu, tunahitaji kushinda na kupata kikombe hiki cha kwanza msimu huu,” alisema Hitimana.

Previous articleKapombe apata pacha
Next articleWAMETISHA
- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa timu hiyo kuwa atajituma na...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi katika klabu ya Simba kwa...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -