Saturday, August 15, 2020

Simba ni mafuriko Sumbawanga

Must Read

Wakili kiboko anunua kesi ya Morrison

NA WINFRIDA MTOI WAKALI aliyejizolea umaarufu nchini kutokana na uwezo na rekodi yake ya...

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa...

NA ASHA KIGUNDULA

KIKOSI cha Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba, leo mchana kinatarajiwa kuondoka jijini Mbeya kwenda mkoani Rukwa, tayari kwa mchezo wao wa fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports (ASFC) dhidi ya Namungo FC.

Mchezo huo wa kukata na shoka unaosubiriwa kwa hamu na wapenzi wa soka nchini, unatarajiwa kuchezwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Nelson Mandela uliopo mjini Sumbawanga.

Habari kutoka ndani ya uongozi wa Simba, zinasema kuwa kikosi chao kitafanya mazoezi ya siku mbili kabla ya mchezo huo.

Simba iliweka kambi yake maalum mkoani Mbeya, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wao huo, ikiwa inahitaji ubingwa wa michuano hiyo.

Kutokana na mkakati wao huo wa kutwaa taji la tatu msimu huu baada ya lile la Ligi Kuu Bara na Ngao ya Jamii, uongozi mzima wa Simba unatarajiwa kutua mjini Sumbawanga ili kuwapa sapoti vijana wao kufanikisha hilo.

Mbali ya viongozi, mashabiki na wanachama kutoka maeneo mbalimbali wamejiandaa kwenda huko kuungana na vijana wao.

Habari kutoka Sumbawanga, zinasema kuwa tayari baadhi ya wapenzi wa Simba wameshatua mjini humo ili kuwahi sehemu za kufikia, huku hoteli na nyumba za wageni zikitarajiwa kufurika kutokana na tukio hilo la kihistoria.

Matawi na makundi ya mitandao ya kijamii ya Simba, tayari wameanza kuhamasishana ili wasafiri kuwafuata vijana wao Sumbawanga kuhakikisha kikosi chao kinarudi Dar es Salaam na ubingwa wa michuano hiyo.

Matawi yanayoonekana kupania safari hiyo ni Simba Jamii, Vuvuzela, Ubungo Terminal, Mpira Pesa, Simba Kigamboni, City Center, Dumila, Simba Msamvu, SDF, Simba Kitunda, Kamati ya Roho Mbaya na mengineyo.

Akizungumza kwa niaba ya Simba Jamii, mlezi wa tawi hilo, Hassan Mbilili, alisema wanachama wao wataondoka kesho asubuhi kwa kutumia usafiri wa badi aina ya Coaster inayobeba watu 28.

Mbilili alisema wana imani na kikosi chao ndiyo sababu ya wao kuwa miongoni mwa wanasimba wanaokwenda Sumbawanga kuipa ushirikiano timu yao.

“Tumejiandaa kuwa miongoni mwa wanasimba watakaokuwepo Sumbawanga, msimu huu ulikuwa mzuri kwetu na tuna uhakika wachezaji wetu hawatatuangusha,” alisema Mbilili.

Kuelekea mchezo huo, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Leonard Wangabo, amewataka wapenzi wa soka kujitokeza kwa wingi katika mkoa wake huo, kwa kuwa wamejipanga kuhakikisha kila kitu kinakuwa sawa.

Alisema maandalizi ya fainali hiyo yapo sawa, wakitarajia kupata wageni kutoka katika mikoa mbalimbali kushuhudia fainali hiyo, ambayo ni mara ya kwanza kufanyika katika mkoa wake.

Simba inacheza na Namungo baada ya kuitoa Yanga katika mchezo wa nusu fainali ilipowachapa watani wao hao wa jadi, mabao 4-1, huku wapinzani wao hao, wakiiondosha Sahare All Stars kwa bao 1-0.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Wakili kiboko anunua kesi ya Morrison

NA WINFRIDA MTOI WAKALI aliyejizolea umaarufu nchini kutokana na uwezo na rekodi yake ya...

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza kupokea maombi kutoka kwa baadhi...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa timu hiyo kuwa atajituma na...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi katika klabu ya Simba kwa...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -