Monday, August 10, 2020

Simba Queens moto wa kuotea mbali

Must Read

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi...

NA GLORY MLAY

SIMBA Queens imeibuka na ushindi mnono wa mabao 7-0 dhidi ya Evergreen katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti Lite, uliochezwa Uwanja wa Karume, jijini Dar es Salaam jana.

Iliwachukua dakika saba Simba kupata bao la kuongoza kupitia kwa Amina Ramadhan kabla ya kuongeza la pili dakika nne baadaye.

Simba waliendelea kilisakama lango la Evergreen na kufanikiwa kupata bao la tatu dakika ya 17 iliyofungwa na Joelle Bukuru ambaye ni raia wa Burundi kwa shuti kali lililogonga mwamba na kuzama wavuni.

Evergreen walijaribu kuonyesha uhai kipindi cha pili lakini walikuwa Simba Queens waliopata bao la nne dakika ya 62 kupitia kwa Amina Ramadhan akimalizia pasi ya Mwanahamisi Omary.

Dakika tatu baadaye, Opah Clement aliitendea haki pasi ya Mwanahamis Omary na kupachika bao la tano kabla ya Mwanahamisi Omary naye kuingia kwenye orodha ya wafungaji akitupia bao la sita dakika ya 76 kwa shuti kali.

Joelle Bukuru alihakikisha Simba Queens wanaondoka na pointi zote tatu baada ya kufunga bao la saba kwa kichwa, akiunganisha pasi ya Amina Ramadhan zikiwa zimebaki dakika tatu mpira kumalizika.

Akizungumza na BINGWA jana, kocha mkuu wa Simba Queens, Mussa Hassan Mgosi, alisema wataendelea kugawa dozi kwa kila timu watakayokutana nayo.

“Tumejipanga mzunguko huu wa pili na tumeweka malengo ya ubingwa hivyo timu zijipange kwani hatutaruhusu kupoteza mchezo kizembe,” alisema.

Naye kocha wa Evergreen, Omary Nyango, alisema uchovu ndio uliowafanya kufungwa lakini wataendelea kupambana kupata matokeo mazuri katika mechi zinazokuja.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa timu hiyo kuwa atajituma na...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi katika klabu ya Simba kwa...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -