Sunday, November 29, 2020

SIMBA SASA IMENOGA SANA, KILA ENEO LINA UTAMU WAKE UWANJANI

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA HUSSEIN OMAR,

MWISHONI mwa wiki iliyopita mashabiki wa soka waliohudhuria mchezo wa ‘Kariakoo derby’ kati ya Simba na Yanga, walipata burudani ya kutosha.

Mbali na matokeo ambapo Simba walichomoza na ushindi wa mabao 2-1, mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ulikuwa kivutio kikubwa kwa dakika zote 90.

Timu zote mbili zilitandaza soka la uhakika kiasi kwamba hata mashabiki wa Yanga walikubaliana na kile kilichotokea huku wale wa Simba nao wakionyesha kuridhika na maamuzi ya mwamuzi Mathew Akrama ya kumpa kadi nyekundu Javier Bokungu.

Kila mchezaji alitekeleza wajibu wake ipasavyo na ni wazi ilikuwa ni moja kati ya mechi bora zilizowahi kuwakutanisha wakongwe hao wa soka la Bongo.

Simba waliwaduwaza wadau wa soka kwa kitendo chao cha kuchomoza na ushindi huo wa mabao 2-1, huku wakiwa pungufu baada ya beki wao wa pembeni, Bokungu kulimwa kadi nyekundu.

Ikumbukwe kuwa wakati Bokungu akipewa kadi nyekundu, tayari Yanga walishatangulia kwa bao 1-0 baada ya kuzawadiwa penalti na mwamuzi Akrama ambaye aliliona wazi kosa la Novaty Lufunga kumkwatua Obrey Chirwa aliyekuwa akielekea kufunga.

Hata hivyo, nini ilikuwa siri ya Simba kushinda mtanange huo licha ya kuwa kwenye wakati mgumu mwanzoni kabisa mwa mchezo?

Ni hivi, Simba ni timu ambayo ukiangalia kikosi chake kimeshamiri vijana wengi wadogo wenye uwezo wa kufanya jambo lolote uwanjani pale inapotokea timu hiyo inataka ushindi.

Ukiangalia umri wa kipa wao Mghana, Daniel Agyei pamoja na kuwa ni mdogo lakini ni moja kati ya makipa wenye uzoefu na michuano mikubwa ndani na nje, kwani msimu uliopita nyanda huyo alisajiliwa na Simba akitokea Medeama FC ya Ghana iliyowatoa jasho Yanga kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho.

Safu ya ulinzi

Ukimwondoa Method Mwanjale ambaye anaweza kuwa ndio mchezaji mwenye umri mkubwa kuliko wote wa Simba, wengine waliobaki ni vijana wadogo ambao wana uwezo wa kumudu kasi yoyote ya mchezo uwanjani.

Abdi Banda, Novaty Lufunga, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’, hawa ni miongoni mwa wachezaji ambao wanaunda safu ya ulinzi ya Wekundu wa Msimbazi ambapo uwezo wao wa kupambana na washambuliaji  na kukaba, kunaifanya Simba kuzidi kunoga kwenye sehemu yake hiyo ya ulinzi.

Kiungo mkabaji na mchezeshaji

Hii ndio sehemu ambayo utawapenda Wekundu wa Msimbazi kutokana na safu hiyo kuundwa na viungo bora wenye uwezo wa kufanya jambo lolote uwanjani na kuamua matokeo ya timu.

Mohamed Ibrahimu ‘Mo’, Jonas Mkude, Said Ndemla, Muzamiru Yasin na James Kotei, hawa ni viungo bora kabisa kwenye ligi kuu msimu huu kutokea kwa Wekundu wa Msimbazi tangu kuondoka kwa kizazi cha akina Athumani Idd ‘Chuji’, marehemu Patrick Mafisango, Christopher Alex na Lubigisa Madata.

Umri mdogo wa viungo hawa unawafanya kufundishika kirahisi na kunasa mafundisho yote wanayopewa na walimu wao lakini pia uwezo binafsi walio nao vijana hawa kunaifanya Simba kuwa timu tishio sana eneo la kiungo msimu huu wa VPL.

Uwezo wa viungo hawa kupanga mashambulizi, kuchezesha timu, kufunga kunaifanya Simba kuwa imara katika idara hiyo ukilinganisha na timu nyingine zinazoshiriki kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.

Safu yao ya ushambuliaji

Safu ya ushambuliaji ya Simba inaundwa na washambuliaji Laudit Mavugo, Ibrahimu Ajib na Juma Luizio. Hawa wote ni moto wa kuotea mbali kwenye kuzifumania nyavu za timu pinzani.

Kwa upande wake Mavugo, usajili wake ulitingisha kwa sababu Simba walimfuatilia kwa muda mrefu na walipokaribia kumnasa alikwenda Ufaransa kufanya majaribio ya soka la kulipwa.

Hata hivyo, nyota huyo hakufuzu na moja kwa moja akatua Simba na kuamsha nderemo na vifijo kwa mashabiki wa klabu hiyo ya Msimbazi.

Hakuchelewa kuonesha makali yake, kwani katika mchezo wake wa kwanza ambao ulikuwa wa ‘Simba Day’, Agosti 8, mwaka jana dhidi ya FC Leopards ya Kenya, alifunga bao moja kwenye ushindi wa mabao 4-0.

Hakuishia hapo, akafunga tena bao moja katika mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ndanda FC na kuiwezesha Simba kushinda mabao 3-1.

Baada ya hapo, mambo yalionekana kwenda kombo kwa straika huyo na kuna kipindi hata mashabiki wa Msimbazi walianza kuchukia walipoona amepangwa kikosini.

Lakini, hivi karibuni Mavugo amerejesha makali yake yaliyowafanya Simba kumfuata Burundi.

Tangu alipoanza kung’ara kwenye kivumbi cha Kombe la Mapinduzi, Mavugo amekuwa moto wa kuotea mbali.

Alikuwa msaada mkubwa wakati Simba iliposhinda mabao 3-0 dhidi ya Majimaji na pia katika ushindi kama huo dhidi ya Tanzania Prisons.

Bao lake katika mchezo dhidi ya African Lyon ndilo lililoipeleka Simba hatua ya robo fainali ya michuano ya FA, huenda timu hizo zingekwenda hatua ya mikwaju ya penalti na kushuhudia Wekundu wa Msimbazi hao wakitolewa, lakini jitihada za Mrundi huyo zikaokoa jahazi. Ukisema Mavugo amerudi utakuwa hujakosea.

Katika mechi za hivi karibuni za Simba, Mavugo na Ibrahim Ajib wameonekana kucheza kwa uelewano wa hali ya juu kiasi cha kutengeneza ‘kombinesheni’ hatari inayowapa jeuri mashabiki wa Simba.

Uwezo wa kupunguza mabeki, kufunga, kupiga pasi za mwisho kunaifanya safu ya ushambuliaji ya Simba kunoga kutokana washambuliaji wote watatu kwa na sifa zinazofanana.

Upana wa kikosi

Mbali na akina Ibrahimu Ajib, Shiza Kichuya, Mohamed Ibrahimu ‘Mo’ , Tshablala, Bokungu, Abdi Banda, Novaty Lufunga, Jonas Mkude, James Kotei, Laudit Mavugo, kuunda kikosi cha kwanza lakini pia kikosi cha pili cha Wekundu hao wa Msimbazi ni moto wa kuotea mbali.

Kikosi cha pili kinaundwa na wachezaji kama Manyika Peter, Hamad Juma, Juuko Murshid, Hija Ugando, Jamal Mnyate, Mwinyi Kazimoto na wengineo  ambao kila anayekaa benchi anakuwa hatari zaidi akiingia uwanjani.

Kutokana na upana wa kikosi hicho ni wazi kuwa Wekundu wa Msimbazi msimu huu wana kila sababu ya kujivunia kuwa na vijana wenye vipaji msimu huu ukilinganisha na misimu mingine iliyopita.

Ushindani wa namba

Kutokana na upana wa kikosi cha Wekundu hao wa Msimbazi kunawafanya wachezaji wa timu hiyo kuwa na ushindani mkubwa wa namba katika kikosi cha kwanza.

Kwenye mazoezi ya timu hiyo utaona kuwa kila mchezaji anafanya mazoezi kwa bidii na kuzingatia mafundisho wanayopewa na walimu wao ili kuwashawishi kuwapa nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

Nyota wa Simba wakiwa mazoezini hawana muda wa kupoteza zaidi ya kuwa bize na mazoezi huku kila mmoja akipambana kwa hali na mali kuhakikisha mwalimu anampa namba ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza.

Benchi la ufundi

Benchi la ufundi la Wekundu wa Msimbazi linaundwa na makocha Joseph Omog na Jackson Mayanja, ambao hawa ni miongoni mwa makocha bora waliowahi kutokea kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara.

Hakuna asiyefahamu uwezo wa Omog ambaye msimu wa 2014 aliipa ubingwa Azam FC kabla ya kutimuliwa kisha baadaye kurejea nchini na kuifundisha Simba.

Kwa upande wake Mayanja, kocha huyo ambaye aliwahi kuzifundisha timu ya Kagera Sugar na Coastal Union ya Tanga, ameonekana kuwa msaada mkubwa kwa Wekundu hao wa Msimbazi tangu arithi mikoba ya kocha msaidizi, Selemani Matola.

Kwa ujumla kama Simba hii ya sasa itakuwa kitu kimoja na kuacha vurugu za hapa na pale za timu hizi kongwe, ni wazi watafika mbali ikizingatiwa kuwa idadi kubwa ya wachezaji wake ni vijana wenye umri wa wastani.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -