Wednesday, August 12, 2020

Simba sasa shwari

Must Read

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi...

NA MWANDISHI WETU

BODO ya Wakurugenzi Simba, imekutana juzi na kufanya mahojiano na benchi la ufundi ili kubaini chanzo cha kudorora kwa kiwango cha timu yao na tayari majibu yamepatikana.

Wajumbe wa bodi hiyo walikutana kuanzia saa moja jioni hadi saa tisa usiku na kumuhoji Kocha Mkuu wa timu hiyo, Sven Vandenbroeck, msaidizi wake, Seleman Matola, Meneja, Patrick Rweyemamu na wengineo.

Viongozi hao wa benchi la ufundi walitakiwa kutoa sababu za kiwango duni cha timu yao na nini kinatakiwa kufanywa ili kikosi hicho kiendelee kuwa tishio kama ilivyokuwa awali.

Kwa mujibu wa chanzo chetu ndani ya bodi hiyo, majibu ya kikao hicho yatawekwa wazi muda wowote kuanzia sasa, huku kukiwa na uwezekano mkubwa wa kutokea mabadiliko ndani ya benchi la ufundi.

Japo wengi wanaamini Sven anaweza kutolewa ‘kafara’ kutokana na mwenendo wa kikosi cha Simba kilichopoteza mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya JKT Tanzania mwishoni mwa wiki iliyopita, lakini imedaiwa kuwa Mbelgiji huyo anaweza kuendelea kupeta na Matola kutemwa.

Matola anadaiwa kuwagawa wachezaji kwa kile anachosisitiza kutopewa ushirikiano na Sven ambaye kila kitu anataka kufanya yeye, yakiwamo majukumu ya mejena Rweyemamu.

Juu ya hilo, mtoa habari wetu amelitonya BINGWA akisema: “Subirini majibu ya kikao cha jana (juzi), lakini sidhani kama kuna ukweli katika hilo…kiufupi hakuna anayefurahishwa na kiwango cha timu hata pale inaposhinda na kocha mkuu ndiye anayewajibika.

“Yeye (Sven) ndiye mwenye jukumu la kuhakikisha timu inashinda na kucheza soka la maana na si msaidizi wake wala meneja, hivyo mambo yakienda kombo, wa kwanza kuulizwa ni kocha mkuu, ipo hivyo hata Ulaya.

“Sven amekuja Simba katika kipindi kibaya sana, ameikuta timu ikiwa inatoka kwenye mafanikio makubwa, imefika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kutwaa ubingwa (wa Ligi Kuu Bara) mara mbili mfululizo, hivyo Wanasimba wanataka zaidi ya hapo, soka maridadi na ushindi mnono,” alisema.

Alisema kuwa kufungwa na JKT Tanzania si sababu pekee inayowatia hasira Simba, bali ni kandanda bovu, tena wakiumizwa zaidi kuona kikosi cha ‘kuungaunga’ cha Yanga kikicheza soka la kueleweka.

“Ila kiukweli, japo kocha (Sven) anaongozana na timu kwenda Morogoro kwa mchezo wetu wa ligi na Mtibwa Sugar, lakini lolote linaweza kutokea na msije kushangaa akiachwa,” alimaliza mtoa habari wetu huyo wa uhakika. 

Lakini wakati hali ikiwa hivyo ndani ya Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, majina mawili yametajwa kuwa njiani kutua katika benchi la ufundi la timu hiyo ili kuokoa jahazi kabla ya kumpata kocha mwingine.

Hao ni mchezaji mwenye rekodi ya kipekee ndani ya Simba, Abdallah ‘King’ Kibadeni na nyota mwingine wa zamani wa timu hiyo, Jamhuri Kihwelu ‘Julio’.

Kibadeni anakumbukwa na wapenzi wa soka hapa nchini kwa kufunga mabao matatu (hat-trick) katika pambano la watani wa jadi, Simba na Yanga, rekodi ambayo haijawahi kuwekwa na mchezaji yeyote Yule.

Kibadeni alifanya hivyo mwaka 1977 wakati Simba ilipoipa Yanga kipigo cha kihistoria cha mabao 6-0.

Mbali ya kung’ara kama mchezaji, Kibadeni pia alifanikiwa kuinoa Simba kwa mafanikio makubwa kama ilivyo kwa Julio. 

Previous articleYANGA NGOMA INOGILE
Next articleTUNAMPENDA
- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa timu hiyo kuwa atajituma na...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi katika klabu ya Simba kwa...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -