Monday, August 10, 2020

Simba SC mambo bam bam

Must Read

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi...

NA WINFRIDA MTOI

SIMBA imejipanga kusomba kila kitu msimu huu bila kuipa nafasi timu nyingine, baada ya kuweka bayana kuwa lazima makombe yote yatue Msimbazi.

Mabingwa hao mara tatu mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, wanatarajia kushuka dimbani kesho kusaka taji la michuano ya Kombe la Shirikisho la Azamb Sports (ASFC) dhidi ya Namungo katika mchezo wa fainali utakaopigwa kwenye Uwanja wa Mandela, mjini Sumbawanga.

Endapo Simba itaibuka bingwa wa michuano hiyo, itakuwa imeweka rekodi ya kuchukua mataji matatu tofauti msimu huu, ikizipoteza Yanga na Azam zilizoshindwa kutamba.

Wekundu wa Msimbazi hao walianza msimu kwa kutwaa taji la Ngao ya Jamii kwa kuifunga Azam FC mabao 3-2 kwenye Uwanja wa Mkapa, jijini Dar es Salaam. 

Kuelekea mechi ya fainali ya ASFC kesho, Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck, ametamba kuwa ni lazima waweke rekodi ya tofauti msimu huu kutokana na kuamini ubora wa nyota wake.

Sven alisema pamoja na hali ya hewa ya Sumbawanga kuwa baridi kali, lakini wachezaji wote wapo katika hali nzuri, huku akiwasisitiza kuvaa nguo nzito.

Alifanunua kuwa kutaka kutimiza malengo yao, ndiyo sababu iliyowafanya wakaweke kambi jijini Mbeya, kujiandaa na mchezo wajua hali ya hewa zinafanana.

“Tunataka kuweka rekodi ya kuchukua mataji muhimu ndani ya msimu mmoja, tayari tumechukua ubingwa wa ligi, bado FA ambao tunacheza siku ya Jumapili (kesho).

“Maandalizi yanaendelea vizuri, wachezaji wote wakiwa katika hali nzuri ingawa hali ya hewa ni baridi, japo si tatizo… tutafanya vizuri. Nafahamu Namungo ni timu bora yenye wachezaji wa viwango vya juu,” alisema Sven.

Naye, Meneja wa timu hiyo, Patrick Rweyemamu, amewataka mashabiki wa timu hiyo kwenda uwanjani wakiwa vifua mbele kuwasapoti wachezaji wao kwa sababu wamejipanga kuondoka na kombe hilo.

“Kama tulivyosema, tunataka kuweka rekodi, tumemaanisha na hatutanii msimu huu ni wetu, kila shabiki aliyepo Sumbawanga na maeneo mengine wasogee karibu, Jumapili tuna jambo letu pale Uwanja wa Mandela,” alisema Rweyemamu.

Wekundu wa Msimbazi hao, juzi walipokewa kifalme na mashabiki waliofurika barabarani baada ya kutua Sumbawanga.

Aidha, inasemekana kati ya mashabiki waliotua Sumbawanga kuitazama timu hiyo, wapo wanaotoka Zambia, nchi ambayo ni jirani na huko, lengo likiwa ni kumwona mchezaji wao, Clatous Chama, akifanya mambo yake.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa timu hiyo kuwa atajituma na...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi katika klabu ya Simba kwa...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -