Saturday, November 28, 2020

Simba ya msimu huu si ya mchezo

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ZAITUNI KIBWANA

SIMBA ya msimu huu si ya mchezo mchezo na hilo limethibitishwa na kasi waliyoanza nayo kwenye Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara pamoja na Kamati kabambe ya watu wanane iliyoundwa ili kuhakikisha hakuna wa kuwazuia kuwa wafalme wa kandanda nchini msimu huu.

Katika kuhakikisha wanaendeleza kasi waliyoanza nayo msimu huu, Simba imeunda kamati hiyo ya mashindano ikiwa imejaa matajiri na watu wanaoweza soka la ndani na nje ya uwanja.

Awali Simba ilikuwa na Kamati ya Mashindano, lakini ilivunjika na sasa wameamua kuunda mpya baada ya kuona umuhimu wa kuwa na kamati hiyo iliyopewa jukumu la kuhakikisha timu inarudisha heshima yake.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Simba, Haji Manara, alisema kamati hiyo mpya ya mashindano itaongozwa na ‘kibosile’ mmoja kutoka kundi la Friends of Simba, Musley Al Ruweh.

Kwa mujibu wa Haji, Musley atakuwa mwenyekiti wa kamati hiyo akisaidiwa na Makamu Wenyeviti wawili ambao ni Hassan Othuman ‘Hasanoo’ (Katibu Mkuu wa zamani wa Simba) na Mohammed Nasoro.

Wajumbe wa kamati hiyo ni Daktari wa zamani wa timu hiyo, Cosmas Kapinga, Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (Taswa), Juma Pinto, Octavian Mushin na Bitulo.

Haji alisema kuwa kazi kubwa ya kamati hiyo itakuwa ni kuhakikisha Simba inashinda michezo yote ikiwemo ya mikoani inayoikabili timu hiyo ili waweze kutwaa ubingwa wa VPL na kurudi kwenye michuano ya kimataifa.

Kuundwa kwa kamati hiyo kunathibitisha jinsi gani Simba imepania kufanya makubwa msimu huu na kupambana na watani wao wa jadi ambao pia karibuni waliunda kamati mpya ya mashindano ikiwa na vigogo kama tajiri Abdallah Bin Kleb.

Katika hatua nyingine, Haji ameitaka kamati ya saa 72 kuweka wazi uchunguzi wanaoufanya ni lini utakamilika ili kuona hatua zitakazochukuliwa dhidi ya mwamuzi Martin Saanya aliyechezesha mchezo wao dhidi ya Yanga.

Alisema anaishangaa kamati hiyo kufuta kadi ya nahodha wao, Jonas Mkude na kumwacha Saanya na wasaidizi wake kwenye uchunguzi ambao anaamini unaweza kutumia hata msimu mzima.

Alisema kufuatia maamuzi mabovu ya Saanya katika mchezo huo, Simba ipo tayari kumlipa mwamuzi kutoka nje ya nchi ili aweze kuchezesha michezo yao mikubwa ukiwemo dhidi ya Yanga.

“Sijawahi kuona uamuzi mbovu kama aliokuwa anaufanya Saanya, hivyo tupo tayari kugharamia gharama zote za mwamuzi kutoka nje ya Tanzania ili aweze kuchezesha mechi yetu na Yanga,” alisema.

Simba wanaongoza msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara wakiwa na pointi 17, walizovuna kwenye michezo saba ya msimu huu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -