Tuesday, October 27, 2020

Simba Ukawa: Tukirudishwa kundini Yanga wamekwisha

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA EZEKIEL TENDWA

UNALIKUMBUKA lile kundi la Simba Ukawa? Sasa limeibuka na kusema kuwa Rais wa klabu hiyo, Evance Aveva, hajatoa kauli ya kuwarudisha kundini na kama atafanya hivyo kabla ya mchezo dhidi ya Yanga, Wanajangwani hao watalia kilio kikubwa.

Simba na Yanga zinakutana Oktoba mosi Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, ambapo kundi hilo la Simba Ukawa limesema wapinzani wao hao ni wepesi sana.

Kiongozi mmoja wa juu wa kundi hilo aliliambia BINGWA kuwa wamekutana na Aveva mara kadhaa wakakubaliana kuwa atawarudisha kundini lakini mpaka sasa yupo kimya na kwamba kama Rais huyo atatoa tamko la kuwarudisha, wapinzani wao watafute pa kutokea.

“Ni kweli mara kadhaa tumekutana na Rais wetu (Aveva) tukafanya mazungumzo ambayo kwa ujumla yalikuwa mazuri sana na alituahidi kwamba yeye kama kiongozi wetu mkuu atafanya mpango aturudishe ili tuwe kitu kimoja.

“Tunaitaka Simba yenye umoja na mshikamano kwani wote tunao uchungu wa kukosa ubingwa misimu minne mfululizo, tunatamani Aveva afanye hivyo kabla ya mchezo wetu na Yanga, wale jamaa (Yanga) wepesi sana,” alisema kiongozi huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe.

BINGWA lilifanya jitihada za kumtafuta Rais huyo wa Simba ili kuzungumzia suala hilo la kuwarudisha kundini wanachama hao ambao walifutiwa uanachama wao baada ya kufungua kesi mahakamani ambapo juhudi hizo ziligonga mwamba.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -