Monday, August 10, 2020

Simba vs Yanga: Haya yataamua mechi ya Kariakoo Dabi

Must Read

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi...

NA MAREGES NYAMAKA

ZIMEBAKI saa chache kabla ya umati wa mashabiki na wadau wa soka nchini na nje ya mipaka ya Tanzania, kushuhudia ‘Derby’ ya Kariakoo kati ya Simba na Yanga itakayopigwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Klabu hizo mbili kongwe zaidi nchini, zitashuka uwanjani huku Yanga ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kuibuka na pointi zote sita za msimu uliopita, lakini msimu huu hali ni tofauti kwa sababu Simba wanaonekana kuwa kwenye kiwango cha juu kutokana na kuanza ligi vizuri kwa kushinda michezo yake mitano kati ya sita, huku ikiongoza ligi kwa kujikusanyia pointi 16 hadi sasa.

Licha ya rekodi hizo na tambo za mashabiki kuongelea ubora wa vikosi hivyo, kuna mambo matano muhimu ambayo yataamua mchezo huo wa kesho.

Saikolojia

Siku zote katika mchezo mgumu kama huu wenye presha kubwa benchi la ufundi, mbali na kuwaandaa wachezaji kiufundi, hutumia muda mwingi kuwatayarisha kisaikolojia kupambana na presha ya pambano.

Hivyo, katika mechi ya kesho wachezaji watakaoweza kuhimili presha ya mchezo na kuwa vizuri kisaikolojia ndio watakuwa na nafasi kubwa ya kuibuka na matokeo mazuri.

Nidhamu

Mara nyingi Kariakoo ‘Derby’ huwa na tensheni kubwa kwa wachezaji, kitu ambacho mara kadhaa huwatoa mchezoni na wanajikuta wanakosa nidhamu ya mchezo.

Hivyo, timu ambayo itakuwa na nidhamu ya juu katika pambano hili ndiyo ina nafasi ya kuibuka kidedea, hivyo basi makocha wanatakiwa kuwaandaa wachezaji wao kutofanya vitendo vya utovu wa nidhamu uwanjani ambavyo vinaweza kuwasababishia kadi na kuiathiri timu, kama ambavyo kadi nyekundu ya Abdi Banda iliiumiza Simba ikafungwa 2-0 katika mchezo kati ya timu hizo msimu uliopita.

Lakini, suala la nidhamu pia linakuja hata kwenye uchezaji, kwani wachezaji uwanjani wanatakiwa kutimiza majukumu yao kwa asilimia 100 kwa sababu kosa dogo kwenye mechi hii litaamua matokeo.

Uzoefu

Kuna wakati wachezaji wenye uzoefu huitajika kwenye mechi kubwa kama hizi kwa sababu mara nyingi huweza kukabiliana na presha ya mchezo na kuamua matokeo wakati ambayo watu hawakutarajia.

Hii inatokana na ukweli kuwa hata timu inapokuwa imezidiwa uwanjani, wanaweza kubadilika na kuwasoma wapinzani wao bila hata ya kupata maelekezo ya kocha na kufanya maamuzi ambayo yanaweza kuibeba timu yake na kuipa ushindi.

Kutumia nafasi za kufunga

Moja ya matatizo makubwa kwenye timu za Tanzania ni kushindwa kutumia nafasi zinapojitokeza kwenye mechi, na wakati mwingine timu hujikuta ikipoteza pambano kwa sababu tu ilishindwa kutumia nafasi ilizozitengeneza.

Tatizo la kushindwa kutumia nafasi za kufunga linaweza lisiiumize timu pale inapocheza na mpinzani dhaifu, kwa sababu itatengeneza nyingi ambazo baadaye watashinda tu.

Lakini, kwenye mechi kubwa kama hii ya Simba na Yanga, ni mara chache sana unakuta timu inatengeneza nafasi nyingi, hivyo klabu ambayo itatumia nafasi chache zitakazotengenezwa ndiyo itakuwa na nafasi kubwa ya kushinda mechi hiyo.

Mbinu na ufundi

Hii ni vita muhimu sana kwenye pambano hilo na ndiyo yenye nafasi kubwa ya kuamua Jiji la Dar es Salaam linakuwa la rangi gani baada ya pambano hilo ambalo litaisimamisha Tanzania kwa dakika 90.

Vita hii itakuwa ni kati ya kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm na yule wa Simba, Joseph Omog, ambao mbinu, ufundi, mabadiliko (sub) pamoja na utetezi wa vikosi vitakuwa muhimu sana katika kuamua timu gani inaondoka na kilio na timu gani inatoka na kicheko.

 

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa timu hiyo kuwa atajituma na...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi katika klabu ya Simba kwa...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -