Wednesday, October 28, 2020

Simba vs Yanga ni Mavugo na Ngoma tu

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA SALMA MPELI

MAKOCHA wa soka nchini wameeleza masuala mbalimbali ya kiufundi katika mchezo wa kesho baina ya mahasimu wa jadi, Simba na Yanga, huku wengi wakiwataja washambuliaji, Laudit Mavugo wa Simba na Donald Ngoma wa Yanga kuwa ni wachezaji wenye turufu muhimu kwa timu zao.

Simba watakuwa wenyeji wa mabingwa watetezi, Yanga kesho katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, ambayo imeteka wadau wengi wa soka kutokana na historia za timu hizo mbili nchini.

Wakizungumza na BINGWA jana kwa nyakati tofauti, makocha hao waliwataja wachezaji kadhaa wa timu hizo ambao wanaweza kubadilisha matokeo kwenye mchezo huo.

Licha ya Ngoma na Mavugo kutajwa sana na kila kocha, lakini pia wapo wachezaji kama Amissi Tambwe, Thaban Kamusoko, Ibrahim Ajib na Shiza Ramadhan ‘Kichuya’ ambao pia wanaunda kombinesheni nzuri nao wanaweza kuamua matokeo ya timu hizo.

Kwa upande wake kocha wa JKT Ruvu, Hamsin Malale ambaye ni timu yake pekee ndiyo haijafungwa na Simba tangu kuanza kwa michuano hiyo msimu huu, alisema Simba ni timu nzuri lakini mchezo huo utakuwa mgumu kwani timu zote zina washambuliaji wazuri.

“Timu zote zina mastraika wazuri na wanaoweza kubadilisha matokeo kwenye mchezo huo, lakini ni ngumu kutabiri ni nani ataibuka na ushindi kwani mechi hii haitabiriki,” alisema.

Naye aliyekuwa kocha wa Ndanda, Hamimu Mawazo, amesema Simba na Yanga zote ni timu nzuri na zina wachezaji wazuri, lakini matokeo katika mchezo huo yatapatikana kwa timu itakayoamka vizuri siku hiyo.

“Unaweza ukajiandaa lakini soka lina mambo mengi kwani siku ukiamka vibaya unaweza kuambulia kichapo hivyo siwezi kutabiri ni nani anaweza kuibuka na ushindi ila timu zote zina wachezaji wanaounda kombinesheni nzuri,” alisema Mawazo.

Kwa upande wake aliyekuwa Kocha Mkuu wa Majimaji ya Songea, Peter Mhina ambaye kwasasa ni msaidizi wa Kali Ongala, alisema timu zote ni nzuri na anaamini zitaweza kutoka na matokeo mazuri lakini inategemea na wachezaji kwani muda wowote wana uwezo wa kubadilisha matokeo.

“Timu zote zinafanya vizuri kikubwa wachezaji wawe makini waepuke makosa na ninaamini kama wachezaji wa timu zote watatulia tutashuhudia pambano zuri sana, watakaotumia vyema nafasi watapata matokeo mazuri,” alisema Mhina.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -