Wednesday, January 20, 2021

SIMBA VS YANGA OKT MOSI  NI SHOO YA KICHUYA NA MAHADHI

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA ZAITUNI KIBWANA

KUELEKEA mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga, homa ya pambano hilo imezidi kupanda baada ya kila timu kumtambia mwenzake.

Zikiwa ni siku chache kabla ya mchezo huo utakaochezwa Oktoba Mosi, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kuna mambo mbalimbali ya kuyaangalia, lakini leo tukiwatupia macho winga wa Simba, Shiza Kichuya na yule wa Yanga, Juma Mahadhi.

Kichuya na Mahadhi wote wameanza kutumikia vikosi hivyo msimu huu baada ya kusajiliwa kutoka Mtibwa Sugar na Coastal Union, ambayo kwa sasa imeshuka daraja.

Mahadhi anajua kutengeneza nafasi, ana kasi, nguvu na ni mwepesi kumwezesha kumiliki mpira kadri anavyotaka, huku akiwa ni mwenye kujiamini mno.

Mahadhi, ambaye ni mjomba wa mchezaji wa zamani wa Yanga, Waziri Mahadhi, alionyesha kiwango cha hali ya juu kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe, ambapo aliweza kushambulia na kukaba, kuanzia wingi ya kulia hadi kushoto, huku akionyesha umahiri wa hali ya juu katika kupiga krosi.

Kiungo huyo, ambaye amepachikwa jina la Kiberenge kwa sababu ya kasi, aliwahi kutakiwa na Simba na baadaye Yanga waliwazidi kete watani wao hao wa jadi na kumtwaa, hivyo Oktoba Mosi atataka kuonyesha kuwa Wanajangwani hao hawakukosea kumsajili.

Kwa upande wao, Simba wana Kichuya ambaye amewahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi inayotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), akiwa na sifa ya kubadili matokeo wakati wowote.

Winga huyo anajiamini na ndiye mchezaji aliyechangia kwa kiasi kikubwa ushindi wa kikosi hicho ambacho kwa sasa kinaongoza kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kichuya ana sifa za kushambulia, anapandisha timu, kukaba, mbio, mkali wa pasi zenye macho na pia ana nguvu za kumwezesha kupambana.

Zaidi ya hayo, Kichuya ni fundi wa kufunga, akiwa ndiye aliyeibeba timu yake ilipocheza na Azam mwishoni mwa wiki iliyopita na kushinda bao 1-0.

Ni kutokana na sifa hizo za wawili hao, mashabiki wanasubiri kwa hamu kuona nani kati ya Kichuya na Mahadhi atakayefanikiwa kung’ara Oktoba Mosi, kwenye Uwanja wa Taifa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -