Friday, November 27, 2020

SIMBA WAIMALIZA AZAM MCHANA KWEUPE

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA EZEKIEL TENDWA

SIMBA wanajua kuwa wanao mchezo mgumu dhidi ya Azam utakaochezwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam na wakiteleza tu, imekula kwao na sasa wameliandaa jeshi lao kuhakikisha wanamaliza mchezo kabla jua halijazama.

Mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa pande zote wakiwamo watani wao wa jadi Yanga ambao wanaombea Simba wafungwe ili waweze kuwaengua kileleni, wanaongoza ligi hiyo kwa pointi 45, wakifuatiwa na wao wenye pointi 43.

Simba wakifungwa mchezo huo na Yanga wakabahatika kushinda dhidi ya Mwadui Jumapili, wekundu hao wa msimbazi watawapisha watani zao wa jadi kileleni katika mchezo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

Kwa kutambua kuwa wanao maadui kila kona, Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog, ameamua kuwapa mazoezi ya nguvu wachezaji wake huku akionekana kuisuka upya safu yake ya ushambuliaji.

Simba ambao wapo kambini Ndege Beach, Mbweni nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, wamekuwa wakijifua vikali katika Uwanja wa Boko Veterani,  ambapo Omog ameonekana kuwasuka kisawasawa vijana wake akikumbuka kuwa walipata kipigo kule Zanzibar michuano ya Mapinduzi.

Katika mazoezi hayo, Omog amekuwa akiwasisitiza mabeki wake kuhakikisha wanakuwa makini kukabiliana na washambuliaji wa timu pinzani wasilete madhara, hiyo ikiashiria kuwa akina John Bocco wa Azam FC wanatengenezewa dawa chungu.

Kwa upande wa viungo, Omog amekuwa akiwaelekeza namna ya kupiga pasi nzuri na za uhakika zitakazowasaidia washambuliaji kuwa na kazi rahisi ya kufunga na pia viungo hao wakitakiwa kuwarahisishia kazi mabeki kwa kuwasaidia kuzuia.

Katika safu ya ushambuliaji, Omog anajua kuwa pamekuwa na idadi ndogo ya mabao ambapo katika mazoezi hayo ameanza kuwasuka upya akina Laudit Mavugo na wenzake kuhakikisha wanaifanyia kitu mbaya Azam katika mchezo huo.

Simba wapo kileleni mwa msimamo wakiwa na pointi 45 wakifuatiwa na Yanga wenye pointi 43 na kama wekundu hao wa msimbazi watakubali kupata matokeo mabaya, watawapa nafasi wapinzani wao hao kuwashusha.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -