Friday, November 27, 2020

SIMBA WAKAZURU KABURI LA MAFISANGO

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA ONESMO KAPINGA

HABARI ndio kama ilivyokuwa kwamba Simba imetoka kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar  ikiwa na ‘mkosi’ kiasi cha kuendelea kufanya vibaya katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Baada ya kufungwa bao 1-0 na Azam katika mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi uliopigwa Januari 13 mwaka huu kwenye Uwanja wa Amaan, Simba juzi walipata kipigo kama hicho kwenye mechi ya ligi kuu iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Kipigo hicho kimekuja baada ya kutoka sare tasa na Mtibwa Sugar mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

Kitu cha kushangaza, Simba wamekuwa wakicheza sana, lakini hawapati matokeo mazuri, sijui tatizo liko wapi?! Ni kocha? Ni wachezaji? Ni uongozi au ‘kukosa bahati’? Kwa kweli sijui na sijui kama nitajua.

Ningali najiuliza kilichowafanya kuwamwaga wafungaji wao bora wa misimu. Ukikumbuka ya Amisi Tambwe kuondolewa kwa madai ya kushuka kiwango, naamini hutashangaa ‘kutoswa’ kwa mkali mwingine Hamisi Kiiza. Cha kushangaza, Tambwe alikuwa bora akiwa Simba na alipohamia Yanga akaendelea kuwa bora. Sijui kiwango chake kilishuka vipi.

Hivi sasa tunafahamu kuwa Kiiza yuko Afrika Kusini akisakata kabumbu, tena kwa mafanikio.

Hebu tujiulize, vipi mastraika wa sasa Laudit Mavugo na Fredrick Blagnon? Dhamira ya kuletwa Simba ni kufungia mabao tu, tena ikibidi kila mechi, lakini bado wameshindwa kuleta matokeo maridhia kama kusudi lilivyo. Kila mmoja ni shuhuda kuwa mabao mengi ya Simba siku hizi yanafungwa na ma-winga na viungo akina Shiza Ramadhan ‘Kichuya’, Yassin Mzamiru, Ibrahim Mohamed ‘Mo’ na Jamal Mnyate.

Mshambuliaji aliyekabidhiwa jukumu la kufumania nyavu amekuwa ‘butu’ kiasi cha kushawishi mashabiki kuwa hana kiwango cha u-proo au hana bahati. Huyu Laudit Mavugo, kashindwa kutoa matunda yanayotakiwa na klabu. Aliweza kuwapa tumaini katika mechi za mwanzo wa ligi msimu huu lakini sasa ‘mweupeee’, masikini, kijana wa watu halioni ‘goli’.

Nikirudi katika kitovu cha makala hii, ni maswali juu ya maswali. Maana tangu Simba ilipopoteza michezo miwili mfululizo ya mwisho wa mzunguko wa kwanza kwa kupigwa bao 1-0 na African Lyon kwenye Uwanja wa Uhuru, kisha mabao 2-1 na Prisons pale Sokoine, Mbeya, hali ilikuwa ‘tete’ na tushukuru Mungu ligi ilikuwa ukingoni mwa mzunguko… bila hivyo sijui nini kingejiri.

Haya, kama haitoshi, wakiwa mapumzikoni, tukashuhudia kipa wao, Vincent Angban, akipandishwa ndege kurudishwa kwao hukooo Ivory Coast. Hakika, mpaka sasa sijajua sababu za ‘kummwaga’ aliyewadakia zaidi ya mechi nane bila timu kupoteza.

Ukiangalia kwa undani kinachoiumiza Simba kwa sasa ni kukosekana mtu wa mwisho (finisher) anayesimama mbele kumalizia kazi za mawinga na viungo, badala yake mabao karibu yote yamekuwa yakifungwa na viungo na mawinga ilhali kuna ‘mtu’ maalumu kwa kazi hiyo. Sio siri, ubutu wa washabuliaji ndio unaoitesa Simba, ukibisha wewe jeuri.

Ndio maana hata kichwa cha habari cha safu hii nimekihusisha na msiba wa aliyekuwa kiungo mahiri wa Simba, marehemu Patrick Mafisango, aliyefariki Mei 17 mwaka 2012. Kivipi? Ni kutokana na matokeo mabaya yanayoendelea kuisakama klabu kwa kukosa ubingwa wa ndani kwa miaka kadhaa na ndio maana hata ushiriki wao kimataifa umepigwa ganzi. Kuna anayebisha?

Uwapo wa Mafisango ndani ya Simba ulikuwa zaidi ya muhimu. Alikuwa nguzo sahihi kwa uwajibikaji wake uwanjani. Lakini namna Simba yenyewe ilivyomtendea baada ya kifo chake ndiyo inayozua minong’ono mitaani kwamba, labda kuna kitu kama klabu lazima kifanyike kuwarehemu wana-Simba wote waliotangulia mbele ya haki kama njia ya kutafuta suluhu ya mikwamo wanayokumbana nayo sasa.

Huu usichukuliwe kama ushirikina au imani potofu, la hasha, tunaona hata Ulaya mara kadhaa wachezaji huvaa vitambaa vyeusi kwa misiba ya wadau na nyakati nyingine kufanya misa au hafla za kuwaombea na kuwakumbuka wapendwa wao.

Kabla ya kujiuliza nini cha kufanya ili kuondokana na zahama hii, lazima ijengwe ari ya ushindi miongoni mwa wana-Simba wote mahali walipo ikianzia ndani ya klabu mpaka mitaani huku wakijisuta kwa ‘hasira’ kuwa kwanini mara ya mwisho Simba kushiriki michuano ya kimataifa ulikuwa mwaka aliofariki Mafisango? Maana, kumbukumbu zinaonyesha ilitolewa na Al Ahly Shandy ya Sudan katika hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho Afrika.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -