Friday, October 23, 2020

Simba wakubali yaishe

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA MARTIN MAZUGWA,

SIMBA wamekubali kulipa gharama za uharibifu wa miundombinu ya Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, baada ya mashabiki wao kung’oa viti katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Yanga, iliyochezwa juzi.

Mkuu wa Idara ya Habari na  Mawasiliano wa Simba, Haji Manara, alisema jana kuwa,  klabu itazungumza na wamiliki ambao ni serikali ili waweze kulipa gharama za matengenezo za uharibifu wa mali  uliotokea.

Haji alisema pamoja na kubeba jukumu hilo, klabu hiyo imeomba radhi kutokana na uharibifu uliofanywa na mashabiki wao.

Alisema  mbali  hilo, leo wanatarajia  kuwasilisha malalamiko kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) juu ya uchezeshaji mbovu wa waamuzi wa mechi hiyo.

Manara alisema haieleweki ni kigezo gani kilitumika kumpa mwamuzi Martin Saanya  kuchezesha mechi hiyo, wakati wanajua uwezo wake.

Mashabiki wa Simba walifanya uharibifu huo kwa lengo la kupinga uamuzi wa Saanya, ambaye alionekana kushindwa kumudu pambano hilo, lililomalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -