Tuesday, October 27, 2020

SIMBA WAKUMBUKA SHUKA KUMEKUCHA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA SALMA MPELI

SIMBA wamekumbuka shuka kumekucha. Kocha msaidizi wa timu hiyo, Jackson Mayanja, amesema wanahitaji kufunga mabao mengi ili waweze kujiweka katika mazingira bora ya kuchukua ubingwa wa msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara, iwapo  utaamuliwa kwa idadi ya mabao.

Mayanja ameonekana kuwashtukia wapinzani wao wa soka, Yanga ambao wanawazidi kwa mabao 10 ya kufungwa, licha ya wao kuongoza katika msimamo wa ligi hiyo kwa pointi 51.

Yanga wamefunga mabao 46 huku Simba wakifunga 36, lakini Wekundu wa Msimbazi wanaongoza katika msimamo wa ligi hiyo kutokana na pointi 51 wakifuatiwa na watani wao wenye pointi 49.

Hata hivyo, Yanga wana mchezo mmoja mkononi, baada ya kucheza mechi 21 na Simba wakiwa wamecheza mechi 22, lakini wakiwa wamefunga mabao machache dhidi ya watani wao.

Kwa kuliona hilo, Mayanja amewataka wachezaji wake kufunga mabao mengi katika mechi moja ili kujiweka kwenye mazingira bora iwapo ubingwa utaamuliwa kwa wastani wa mabao ya kushinda na kufungwa.

Mayanja alisema wana kazi kubwa ya kuhakikisha wanashinda kwa idadi kubwa ya mabao katika mechi zao zilizosalia ili kula sahani moja na Yanga.

“Kutokana na kuwa mwenendo wa ligi  kwa sasa bingwa anaweza kupatikana kwa idadi ya mabao, hivyo lazima tushinde mabao mengi,” alisema.

Simba walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tanzania Prisons uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam huku Mayanja  akisema ni mikakati yao ya kutwaa ubingwa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -