Saturday, January 16, 2021

SIMBA WASIPOSHTUKA, AGOSTI 23 WATALIA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

 NA EZEKIEL TENDWA

BENCHI la ufundi la Simba liligundua kwamba walikosa ubingwa msimu uliopita kutokana na safu yao ya ushambuliaji kushindwa kufunga mabao mengi na kuzidiwa na Yanga, hivyo kuamua kufanya usajili wa nguvu ili kutatua tatizo hilo la mabao.

Lakini pamoja na hilo, tatizo hilo limeonekana liko pale pale, kutokana na hali ilivyojionyesha ndani ya mechi nne za kirafiki za timu hiyo kujiandaa na msimu mpya.

Ndani ya mechi hizo, Simba imefunga mabao matatu tu, tofauti na Yanga ambao nao wamecheza idadi hiyo ya mechi za kirafiki na kuvuna mabao tisa.

Msimu huo uliopita Simba walimaliza ligi wakiwa na pointi 68, sawa na Yanga, lakini wakaukodolea macho ubingwa ukibaki Jangwani, baada ya kuzidiwa kwenye wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa, wao wakifunga mabao 50 na watani zao hao wa jadi wakitumbukiza nyavuni mabao 57.

Tatizo kubwa lililokuwa linawakabili Simba ni kutokana na safu ya ushambuliaji iliyokuwa ikiongozwa na Laudit Mavugo, Ibrahim Ajib, Frederick Blagnon, pamoja na Juma Luizio, kushindwa kufunga mabao ya kutosha, tofauti na ile ya Yanga chini ya Amis Tambwe, Donald Ngoma, Obrey Chirwa na Simon Msuva, ambao walikuwa hawatanii wanapokuwa mbele ya lango la timu pinzani.

Hilo ndilo lililomshtua Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog na wasaidizi wake, hivyo kuamua kusajili washambuliaji wenye uchu wa mabao, ambao ni John Bocco, Emmanuel Okwi na Nicholas Gyan kutoka Ghana, ambao wameungana na Shiza Kichuya, Laudit Mavugo na Juma Luizio.

Nyuma ya washambuliaji hao, kuna kiungo mpya, Haruna Niyonzima, aliyetokea Yanga, ambaye ameungana na waliokuwapo kikosini, Muzamiru Yassin, Mohammed Ibrahim ‘Mo’, Said Ndemla na Jonas Mkude.

Pamoja na usajili huo, bado benchi la ufundi la Simba linatakiwa kufanya kazi ya ziada, kwani tatizo linaonekana lipo palepale, tofauti na ilivyo kwa Yanga, wanaoonekana kuwa na moto uleule wa kufunga mabao mengi.

Udhaifu wa safu ya ushambuliaji ya Simba, umeonekana katika michezo yao ya kirafiki waliyocheza mpaka sasa, kitu ambacho kinaendelea kuwapa presha mashabiki wao, ambao wanashuhudia upande wa pili ukifanya kweli.

Katika michezo yao minne ya kirafiki, Simba wamefunga mabao matatu, huku Yanga wakicheka na nyavu mara tisa ndani ya idadi hiyo ya mechi.

Katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini, Simba walifungwa bao 1-0, kabla ya sare ya bao 1-1 na Bidvest Wits na hatimaye kushinda bao 1-0 walipovaana na Rayon Sports ya Rwanda, katika mchezo wa tamasha la Simba Day, huku wakishinda bao 1-0 juzi dhidi ya Mtibwa Sugar.

Kwa upande wao, Yanga walishinda mabao 5-0 dhidi ya timu ya Chuo cha Biblia Morogoro, wakashinda tena mabao 3-2 dhidi ya Singida United, kabla ya kufungwa bao 1-0 na Ruvu Shooting na kukimbilia Zanzibar, walikocheza na Mlandege na kutoka na ushindi wa mabao 2-0.

Tatizo kubwa linaloonekana kuigharimu safu ya ushambuliaji ya Simba ni kushindwa kutumia vizuri nafasi wanazozipata, tofauti na wenzao wa Yanga, huku winga wao, Shiza Kichuya, akianza kulalamikiwa kutokana na uchoyo wa kutoa pasi kama ilivyojionyesha kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar juzi.

Simba wanaonekana kuwa na safu kali ya ulinzi, ambapo katika michezo hiyo minne ya kirafiki, imeruhusu bao moja tu, huku ile ya Yanga ikiruhusu mabao matatu, hali hiyo ikimaanisha kuwa kazi kubwa ya Omog ni kunoa zaidi safu yake ya ushambuliaji kuhakikisha inafunga mabao mengi, huku Kocha wa Yanga, George Lwandamina, akiwa na kazi kuisuka upya safu ya ulinzi.

Jambo la kufurahisha kwa mashabiki wa Simba ni kwamba, tayari kocha wao msaidizi, Jackson Mayanja, amekiri kugundua tatizo la safu yao ya ushambuliaji na kuahidi kulifanyia kazi haraka iwezekanavyo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -